Mkuu wa MkoaMhe Dkt. Rehema Nchimbi

HABARI NA MATUKIO

MKOA WA SINGIDA

Jamii: Homepage Imechapishwa: Jumatatu, 06 Juni 2016 Imeandikwa na Super User

Ndugu Msomaji Karibu katika tovuti rasmi ya Mkoa wa Singida. Mkoa wa Singida upo katikati ya Tanzania Bara. Mji wake Mkuu ni Singida na ni njia panda muhimu kwa usafiri wa barabara kwenda Kaskazini, Magharibi, Kusini na Mashariki.

Singida inapakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kaskazini, Mkoa wa Dodoma upande wa Mashariki, Mikoa ya Mbeya na Iringa upande wa Kusini na Mikoa ya Tabora na Simiyu upande wa Magharibi.

Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi tarehe 15 Oktoba, 1963 ambapo kabla ya hapo ulikuwa ni Wilaya ya Jimbo la Kati (Central Province) uliojumuisha Mkoa wa Dodoma.

Mkoa wa Singida uko katikati ya Tanzania, kati ya Longitudo 33027’5’’ na 35026’0’’ mashariki ya Greenwich, na kati ya latitudo 3052’ na 7034’ Kusini mwa Ikweta.

Mkoani Singida ndipo kuna eneo eneo rasmi ambalo lilibainishwa na vipimo vya kitaalamu vyenye namba 9305404.35, 698978.015 kuwa ni katikati mwa Tanzania bara yaani Central point of Tanganyika, ambapo ni katika kitongoji cha Darajani, Kijiji cha Chisingisa kilichopo kata ya Sasilo, tarafa ya Nkonk’o Wilaya ya Manyoni.

Mkoa wa Singida una Wilaya 5 ambazo ni  Singida, Iramba, Manyoni, Mkalama na Ikungi; zenye Halmashauri 7 za Singida, Singida Manispaa,  Iramba, Manyoni, Mkalama, Ikungi na Itigi. Aidha Mkoa una Tarafa 21, kata 136, Vijiji 442, vitongoji 2,309 na majimbo ya uchaguzi 8.

Ukubwa wa eneo la Mkoa wa Singida ni kilomita za mraba 49,341 sawa na asilimia 6 ya eneo la Tanzania Bara ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 11,340 zinafaa kwa kilimo sawa na asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa. 

Soma zaidi/ ReadMore

Mavumbuo: 7734