• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Historical Background

Ndugu Msomaji Karibu katika tovuti rasmi ya Mkoa wa Singida. Mkoa wa Singida upo katikati ya Tanzania Bara. Mji wake Mkuu ni Singida na ni njia panda muhimu kwa usafiri wa barabara kwenda Kaskazini, Magharibi, Kusini na Mashariki.

Singida inapakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kaskazini, Mkoa wa Dodoma upande wa Mashariki, Mikoa ya Mbeya na Iringa upande wa Kusini na Mikoa ya Tabora na Simiyu upande wa Magharibi.

Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi tarehe 15 Oktoba, 1963 ambapo kabla ya hapo ulikuwa ni Wilaya ya Jimbo la Kati (Central Province) uliojumuisha Mkoa wa Dodoma.

Mkoa wa Singida uko katikati ya Tanzania, kati ya Longitudo 33027’5’’ na 35026’0’’ mashariki ya Greenwich, na kati ya latitudo 3052’ na 7034’ Kusini mwa Ikweta.

Mkoani Singida ndipo kuna eneo eneo rasmi ambalo lilibainishwa na vipimo vya kitaalamu vyenye namba 9305404.35, 698978.015 kuwa ni katikati mwa Tanzania bara yaani Central point of Tanganyika, ambapo ni katika kitongoji cha Darajani, Kijiji cha Chisingisa kilichopo kata ya Sasilo, tarafa ya Nkonk’o Wilaya ya Manyoni.

Mkoa wa Singida una Wilaya 5 ambazo ni  Singida, Iramba, Manyoni, Mkalama na Ikungi; zenye Halmashauri 7 za Singida, Singida Manispaa,  Iramba, Manyoni, Mkalama, Ikungi na Itigi. Aidha Mkoa una Tarafa 21, kata 136, Vijiji 442, vitongoji 2,309 na majimbo ya uchaguzi 8.

Ukubwa wa eneo la Mkoa wa Singida ni kilomita za mraba 49,341 sawa na asilimia 6 ya eneo la Tanzania Bara ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 11,340 zinafaa kwa kilimo sawa na asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa. 

Kwa upande wa hali ya hewa Mkoa wa Singida hupata mvua kwa kipindi kimoja cha mwaka (mwezi Novemba hadi Aprili) kwa wastani wa milimita 500 – 800 kwa mwaka na  wastani wa hali ya hewa ni nyuzi joto 15 – 30 kutegemea msimu na mwinuko wa ardhi. Kutokana na hali ya hewa, Mkoa wa Singida ni miongoni mwa Mikoa iliyopo kwenye ukanda wa unaopata mvua kidogo.

Kwa miaka ya karibuni wastani wa mvua umekuwa ukipungua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kote Duniani.  Kwa mfano mwaka 2008/2009 kiasi cha mvua kilichorekodiwa katika kituo cha hali ya hewa Singida ni mm 778, mwaka 2009/2010 mm 641 na  mwaka 2010/2011 mm 425.7, mwaka 2011/2012 mm 582 na mwaka 2012/2013 mm 821.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Singida ni 1,370,637 ikiwa wanaume ni 677,995 na wanawake ni 692,642 huku kaya zikikadiriwa kuwa 225,670 ambapo kaya 189,115 zinajishughulisha na kilimo.

Shughuli za kiuchumi Mkoani Singida ni pamoja na kilimo ambacho huajiri wastani wa asilimia 86 ya wakazi wote. Mazao ya kipaumbele kwa upande wa chakula ni uwele, mtama, mihogo na viazi vitamu  na kwa upande wa mazao ya biashara ni alizeti, vitunguu, pamba na ufuta. Shughuli nyingine za uzalishaji mali ni ufugaji, uchimbaji mdogo wa madini, viwanda vidogo na biashara.

Pato la Mkoa ni Sh. 978,701,000 huku pato la mwananchi likiwa ni Sh. 697, 667 kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2013.

Uongozi na Utawala wa Mkoa umekuwa ukibadilika mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya Kitaifa. Tangu Mkoa uanzishwe hadi sasa Mkoa umeongozwa na jumla ya Wakuu wa Mikoa 18 kwa vipindi tofauti.    

Orodha ya Wakuu wa Mikoa waliofanya kazi Mkoani Singida tangu uanzishwe ni kama ifuatavyo:

Na
Jina
Mwaka
Picha
1
Bw. Dantes Ngua
1963 – 1964

2
Bw. Peter Kisumo
1964 – 1965

3
Bw. Rajabu Semvua
1965 – 1969

4
Bw. Kapilima Kapilima
1969 – 1971

5
Bw. Kingunge N. Mwiru
1971 – 1972

6
Bw. Moses Nnauye
1972 – 1975

7
Bw. Charles Kileo
1975 – 1977

8
Brigedia Silas Mayunga
1977 – 1978

9
Bw. Abdallah Nungu
1978 – 1981

10
Capt. Peter N. Kafanabo
1981 – 1986

11
Prof. John B. Machunda
1986 – 1987

12
Maj. Gen. Mwita C. Marwa
1987 – 1990

13
Bw. Gallus N. Abedi
1990 – 1993

14
Bw. Abubakary Y. Mgumia
1993 – 1997

15
Col. Anatoli N. A. Tarimo
1997 – 2002

16
Bibi Halima Y. Kasungu
2002 – 2006

17
Dkt. Parseko V. Kone
2006 –2016

18
Mhe. Mathew J. Mtigumwe
Machi 2016- Disemba 2016

19
Dkt. Rehema Nchimbi
Disemba 2016 - Mei 2021

20
Dkt. Binilith Saatano Mahenge
Mei 2021 - Julai 2022

21
Mhe. Peter Joseph Serukamba
Aug 2022 hadi sasa


Kwa upande wa ngazi ya Mtendaji Mkuu wa Serikali katika Mkoa, Serikali ya Mkoa imekuwa inaongozwa na Wakurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa tangu mwaka 1972 na baadaye mwaka 1997 chini ya Sheria Na. 19 ya Tawala za Mikoa – (Regional Administration Act Na. 19)  Makatibu Tawala wa Mikoa (Regional Adiministrative Secretaries – RAS) waliteuliwa kuongoza Sekretarieti za Mikoa ikiwa ni njia ya kuimarisha uwajibikaji na utoaji huduma bora kwa wananchi.

Wakurugenzi wa Maendeleo walioongoza Mkoa tangu 1972 ni kama ifuatavyo:-

1.     Bw. M. Jabiri Kigoda        1963 – 1964

2.     Bw. C. M. Joachim   1972 – 1974

3.     Bw. C. L. Kombo      1974 – 1975

4.     Bw. Crispin Duncan Mbapila   1976 – 1977

5.     Bw. I. Abubakar       1978 - 1983

6.     Bw. L. M. Rimisho   1984 – 1985

7.     Bw. A. S. Kaduri      1985 – 1988

8.     Bw. A. A. K. Mwasajone   1988 - 1989

9.     Bw. T. N. Machume 1989 – 1991

10.   Bw. Fredrick Nyelwa Kisenge   1991 – 1994

11.   Bw. Alfred Francis Fuko  1994 – 1995

12.   Bw. Emanuel Petro Mazalla     1995 – 1997

Makatibu Tawala wa Mkoa waliouongoza Mkoa tangu mwaka 1997 ni kama ifuatavyo:-

1.     Bw. Martin Odilo Mgongolwa   1997 – 2004

2.     Bw. Zawadiel Mchome     2004 – 2006

3.     Bibi Dyness G. Senyagwa 2006 – 2007

4.     Bw. Hussein A. Kattanga 2007 – 2009

5.     Bw. Godfrey S. Ngaleya    2009 – 2010

6.     Bw. Liana A. Hassan        2010 – 2015

7.    Bw. Festo L. Kang’ombe    2015- 2016

 8.    Dkt. Angelina M. Lutambi   May 2016 - Juni 2021.

9.  Bi. Dorothy Aidan Mwaluko Juni 2021 - Machi  2023

10. Dkt Fatuma Ramadhan Mganga  Machi 2023 hadi sasa





Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.