• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Local Government


SEHEMU YA SERIKALI ZA MITAA

Sehemu ya menejimenti ya huduma za Serikali za Mitaa ni miongoni mwa sehemu/kitengo katika muundo wa uongozi katika Sekretarieti ya Mkoa ambayo kazi yake kubwa ni kutoa ushauri wa kitaalam, kusimamia utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za mitaa katika nyaja za utawala bora, usimamizi wa makusanyo ya mapato ya ndani na matumizi ya fedha za umma, utekelezaji wa sheria za nchi na sheria ndogo za Halmashauri, masuala ya kiutumishi na uandaaji wa Mipango na Bajeti.

Sehemu ya Menejimenti ya Huduma za Serikali za mitaa inaongozwa na Bw. Evodius R. Katare -   Katibu Tawala Msaidizi anayehusika na usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Singida

PICHA YA KATIBU TAWALA MSAIDIZI

 

MAENEO YA USIMAMIZI

Sehemu ya Serikali za Mitaa inazisimamia Halmashauri saba za Mkoa wa Singida ambazo ni Halmashauri za Wilaya ya Ikungi, Iramba, Itigi, Manyoni, Mkalama, Singida na Halmashauri ya Manispaa ya Singida. Halmashauri hizi zipo katika Wilaya tano (5) za Mkoa wa Singida ambazo ni

  • Wilaya ya Iramba (Halmashauri ya Wilaya ya Iramba),
  • Wialaya ya Mkalama (Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama),
  • Wilaya ya Manyoni (Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na Itigi),
  • Wilaya ya Ikungi (Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi) na
  • Wilaya ya Singida (Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Manispaa ya Singida)

Halmashauri za Wilaya zinaongozwa na Wenyeviti wa Halmashauri na Halmashauri ya Manispaa inaongozwa na Mstahiki Meya. Watendaji wakuu wa Halmashauri za Wilaya ni Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri na mtendaji mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ni Mkurugenzi wa Manispaa. Halmashauri hizo zina  Tarafa, Kata, Vijiji na vitongozi kama ifuatavyo:

  • Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi (Tarafa 4 ,Kata 28, Vijiji 101 na Vitongoji 539)
  • Halmashauri ya Wilaya ya Iramba (Tarafa 4, Kata 20, Vijiji 70  na Vitongoji 393)
  • Halmashauri ya Wilaya ya Itigi (Tarafa 1, Kata 13, Vijiji 70 na Vitongoji 172)
  • Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni (Tarafa 4, Kata 19, Vijiji 58 na Vitongoji 279)
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama (Tarafa 3, Kata 17, Vijiji 70 na Vitongoji 288)
  • Halmashauri ya Wilaya ya Singida (Tarafa 3, Kata 21, Vijiji 84 na Vitongoji 435)
  • Halmashauri ya Manispaa ya Singida (Tarafa 2 ,Kata 18, Mitaa 53, vijiji 19 na Vitongoji 83)

MAJUKUMU YA SEHEMU YA MENEJIMENTI YA HUDUMA ZA SERIKALI ZA MITAA

Majukumu ya Sehemu ya Menejimenti ya Huduma za Serikali za Mitaa ni pamoja na:-

  • Kiungo kati ya Sekretareiti ya Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa katika masuala ya Usimamizi wa Fedha, Sheria, Kazi (Labour Issues), Utumishi Na Utawala, Uandaaji Wa Mipango na Bajeti.
  • Kufanya ukaguzi wa kawaida na dharura kuhusu utendaji wa Halmashauri.
  • Usimamizi wa Mikataba ya Huduma kwa Wateja ya Halmashauri.
  • Kuhakikisha kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa.
  • Kuhakikisha Halmashauri zinatumia fedha vizuri kwa kuzingatia miongozo iliyopo ya fedha.
  • Kuhakikisha Halmashauri zinakaguliwa na Wakaguzi wa Nje na Ndani ya Halmashauri ili zikidhi viwango vya uandaaji wa Hesabu za mwaka vilivyowekwa, kufuata taratibu na miongozo ya malipo, manunuzi, mikataba n.k.
  • Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Nyanja mbalimbali na kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa dhana ya Utawala Bora kuanzia ngazi za msingi (Vijiji, Mitaa, Vitongoji) hadi Halmashauri.
  • Kuratibu/kuziratibu Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendesha na kusimamia Uchaguzi wa Viongozi wa ngazi za Msingi (Vijiji, Mitaa na Vitongoji) na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, pamoja na chaguzi ndogo kwa kadri zinavyojitokeza.
  • Kuzisimamia na kuzifuatilia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa na kuhuisha rasimu za Sheria Ndogo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya uendeshaji wa Halmashauri baada ya kuidhinishwa na Waziri Mwenye Dhamana na Serikali za Mitaa.
  • Kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zitekeleze majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali kwa maslahi ya ustawi wa wananchi wake.
  • Kuziandaa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuambatana nazo zinapoitwa kushiriki vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa kwenye kuwasilisha Hesabu za mwaka husika uliokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

MAFANIKIO YA SEHEMU YA SERIKALI ZA MITAA KWA MWAKA 2021/2022

  • UTAWALA BORA

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi na Kata zake

Na
Wilaya
Jimbo la Uchaguzi
Halmashauri
Idadi ya Tarafa
Idadi ya Kata
1.
Singida
Singida Kaskazini
Singida DC

03

21

Singida Mjini
Singida MC

02

18

2.
Manyoni
Manyoni Mashariki
Manyoni DC

04

19

Manyoni Magharibi
Itigi DC

01

13

3.
Iramba
Iramba Magharibi
Iramba DC

04

20

4.
Mkalama
Iramba Mashariki
Mkalama DC

03

17

5.
Ikungi
Singida Mashariki

Ikungi DC

02

13

Singida Magharibi

02

15


Jumla
 
 

21

136

NB: Majimbo yote nane (8) yanaongozwa na CCM. Pia kuna wabunge 2 wa viti maalum CCM

Idadi ya Waheshimiwa Madiwani wa Kata na Viti maalum

Na
Halmashauri
Idadi ya Madiwani wa Kata
Idadi ya Madiwani wa Viti maalum
Jumla
1.
Singida DC

21

7

28

2.
Manynoni DC

19

7

26

3.
Iramba DC

20

7

27

4.
Mkalama DC

17

6

23

5.
Ikungi DC

28

10

38

6.
Itigi DC

13

5

18

7.
Singida MC

18

6

24


Jumla

136

48

184

NB: Madiwani wa Kata wanawake wapo 04 kati ya 136 sawa na asilimia 2.9 ya madiwani wa Kata. Kata hizo ni Sepuka (Ikungi), Shelui (Iramba), Itigi Majengo (Itigi), na Majengo (Singida Manispaa).

Madiwani wa Kata CCM-135 na CHADEMA 01.

  • USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA

Katika eneo hili Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zilipata HATI INAYORIDHISHA katika ukaguzi uliofanywa kwa mwaka 2020/2021 na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

  • UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI

Halmashauri za Mkoa wa Singida zimepewa mamlaka ya kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vilivyopo katika Halmashauri hizo, Chanzo kikubwa cha mapato katika Halmashauri za Mkoa wa Singida ni chanzo cha ushuru wa mazao ambapo asilimia 80 ya wakazi wa Mkoa wa Singida wanajishughulisha na kilimo. Kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni, 2022 jumla ya sh 13,641,188,076.13 zimekusanywa kati ya lengo la kukusanya sh. 16,881,647,081.00 sawa na utekelezaji wa asilimia 81. Mchanganuo ufuatao unaonesha utekelezaji kwa kila Halmashauri:

  • USHIRIKISHAJI WA JAMII KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO 

Ushirikishwaji wa wananchi katika ushiriki na utekelezaji wa uandaaji wa Bajeti kwa ngazi za vijiji na kata pamoja na utekelezaji wa Miradi ya maendeleo unafanyika kwa kutumia Mpango wa Fursa na Vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa (Improved O&OD) ambapo kwa Mkoa wa Singida mpango ulianza kutekelezwa rasmi mwezi Julai, 2017 kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa viongozi wa Mkoa na Halmashauri hasa waheshimiwa Madiwani, wakuu wa idara na vitengo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Maafisa Ugani wa Kata (Maafisa Maendeleo ya jamii, maafisa mifugo na maafisa kilimo) ambapo baada ya mafunzo hayo wananchi wa Mkoa wa Singida walielimishwa pia kuhusu umuhimu wa ushiriki wao katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili kuweza kutatua kwa urahisi changamoto zinazowakabili, kuwa na umiliki na uendelezaji wa Miradi hiyo.

Mafanikio yaliyopatikana katika ushirikishwaji wa jamii ni kama ifuatavyo:

  • Jumla ya Halmashauri saba za Mkoa wa Singida, Kata na Vijiji kumi nne (14) vinatekeleza mpango wa fursa na vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa ambavyo ni kama ifuatavyo:
  • Halmashauri ya Manispaa ya Singida Kata ya Mtipa na Kisaki. Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Kata ya Old Kiomboi na Mgongo.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Kata ya Nkalakala na Miganga
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kata ya Ihanja na Iglansoni.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kata ya Makutupora na Solya.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kata ya Tambukareli na Mitundu.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Singida kata ya Ntonge na Mughunga.
  • Wananchi wa Kata hizo wanaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ifuatavyo:-
  • Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katika shule shikizi cha Mwaghumphi Kata ya Mtipa Manispaa ya Singida

  • Picha kutoka kushoto vyumba vya madarasa na ofisi vilivyojengwa na wananchi wa Kata ya Mtipa, na picha inayofuata Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa akipokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo kutoka kwa mjumbe wa serikali ya kijiji cha Mtipa.
  • Ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule shikizi katika kijiji cha Ntonge, Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katika shule shikizi ya kijiji cha Ntonge, Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

  • Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Makutupora.

Picha kutoka kushoto inaonyesha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi unaoendelea katika shule ya Msingi Makutupora, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na picha inayofuata inaonyesha Katibu Tawala wa Mkoa Singida akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa viongozi wa Kijiji cha Makutupora.

         

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.