• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

HUKU VETA,KULE ZAHANATI MKALAMA KUMEKUCHA

Posted on: October 24th, 2024

Mkoa wa Singida umeendelea kupiga hatua kubwa kwa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati na vyuo vya VETA kila wilaya huku miongoni mwake ikiwa Chuo cha Veta kinachojengwa katika wilaya ya Mkalama kinachogharimu zaidi shilingi Bilioni 1 na milioni 300

Waziri Silaa Wakati akitembelea mradi wa chuo hicho amesema zamani mkoa Singida ulikuwa na chuo kimoja ambacho kiliwalazimu wazazi kutembea umbali mrefu kutafuta nafasi ya watoto kusoma kisha mahali pakuishi wakati wa masomo na gharama za kujikimu tofauti na sasa hivi vyuo hivyo vimejengwa katika kila wilaya na gharama zitapungua sana.

Aidha amewataka wazazi kusimamia malezi na maadili ya watoto ili kuzalisha jamii iliyo bora ili vijana wa Mkalama kuja kufaidi matunda ya chuo kinachojengwa katika kijiji cha mwando na kuwanufaisha Wakazi wanaoshi jirani na chuo hiko

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amesema nje na mipango iliopo katika ujenzi huo wao kama mkoa wanatarajia kuanza ujenzi wa majengo mawili ya mabweni kuanzia mwezi januari mwakani ili kuwarahisishia wanafunzi wanaotaka kusoma chuo hiko kutoka maeneo ya Mbali

Dendego amewahamasisha wananchi kushiriki katika kutoa nguvukazi katika baadhi ya kazi ikiwemo kukusanya mawe na kokoto ili inapofika mwezi wa kwanza ujenzi rasmi wa m

"Sisi kama mkoa tutajiongeza kwa maana ya kuweka mabweni hapa wilaya hii ni kubwa, watakuja watoto watembea kwa miguu lakini wanaotoka kata nyingine lazima walale, mapema januari tunaanza ujenzi wa mabweni”

Loti Kambi mwananchi wa Nkalakala amewataka wazazi na wananchi wenzake kulinda maadili ya watoto wao hasa chuo hiko kitakapoanza kutoa mafunzo kwenye kipindi hiki cha mmomonyoko wa Maadili

“Mimi nawaita wazazi nawapa wito ili tuweze kulea maadili yaweze kuwa mazuri ili tuweze kupata watu wazuri kuja kujifunza hapa”

Katika hatua nyingine Akiwa katika ziara hiohio wilayani humohumo  Jerry Silaa amezindua zahanati ya Kijiji cha Igonia wilayani Mkalama mkoani Singida iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2013 na baadae serikali kumalizia ujenzi wa zahati hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 80.

       Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Silaa amesema zahanati hiyo imejibu kiu ya changamoto ya wananchi waliokuwa wakikumbana nayo kwa kufuata huduma za afya umbali wa zaidi ya kilomita 10

Amesema zahanati hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia kuwahudumia wananchi ili kutokwenda katika maeneo mengine ya mbali kufuata huduma

Zahanati hiyo ilifunguliwa mwezi wa sita mwaka huu (2024) mpaka sasa imehudumia wakazi  880 huku mpango wa kuongeza wahudumu wa afya katika zahanati ukiwekwa ili kurahisisha huduma kwa wananchi.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.