• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

AZIMIO LA DAR ES SALAAM KUCHOCHEA UWEKEZAJI NCHINI

Posted on: January 29th, 2025

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ina uwezo wa kuuza umeme nje ya nchi kwa sababu mahitaji ya umeme nchini hadi kufikia mwezi Novemba mwaka 2024 yalikuwa  megawati 1,888 wakati uzalishaji ulikuwa megawati 3,431.

Rais Samia ameyasema hayo Januari 28, 2025 alipokuwa akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) mkoani Dar es Salaam. 

Aidha, ameweka bayana kuwa moja ya mipango ya Tanzania hivi sasa ni kuunganisha mtandao wa umeme uliopo nchini na nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika ili biashara ya umeme iwezeshwe kutoka Afrika Kusini hadi Misri ambapo tayari imekwishaunganishwa miundombinu ya umeme kwa nchi za Burundi, Kenya na Rwanda huku kwa nchi za Zambia na Uganda utaratibu wa kuziunganisha ukiendelea.

Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania umewakutanisha Marais na Wakuu wa nchi barani Afrika ili kuja na azimio la pamoja la kuwafikishia nishati ya umeme waafrika zaidi ya milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

Kadhalika,Viongozi mbalimbali wa Kimataifa wamesema wanaunga mkono jitihada za kusambaza nishati ya umeme barani Afrika kupitia ajenda ya Mission 300 itakayopeleka umeme kwa watu milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa nishati Afrika,viongozi hao wameeleza mipango ya taasisi zao katika kuchangia kufanikishwa kwa ajenda hiyo huku  wakichangia mjadala maalumu uliokuwa ukiangazia mchango wa taasisi na Jumuiya za kimataifa katika kuleta mapinduzi ya nishati barani Afrika.

Baadhi ya viongozi hao ni Bjorg Sandkjer ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Rachel Kayte ambaye ni Mwakilishi wa masuala ya tabianchi kutoka nchini Uingereza na Woohchong Um ambaye ni Mtandaji Mkuu wa Taasisi inayoshughulikia  masuala ya nishati ya Global Energy Alliance for people and Planet.

       Pia,Wakuu wa Nchi za Afrika ikiwemo serikali ya Tanzania wamepitisha Azimio la Dar es Salaam lenye malengo mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto ya Nishati na kutekeleza mpango wa matumizi ya nishati safi pamoja na ajenda ya ‘Mission 300’ inayolenga kupeleka umeme kwa Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

Azimio hilo ni mkataba wa pamoja wa Wakuu hao wa nchi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya nishati kwa kuhakikisha nishati inakua toshelevu katika mataifa ya Afrika jambo ambalo litachochea uwekezaji katika sekta mbalimbali na kuleta maendeleo.

Aidha, malengo mengine ya azimio hilo ni kuimarisha na kuboresha miondombinu ya nishati pamoja na kufikisha umeme kwa waafrika kwa gharama ndogo, kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya umeme ikiwemo jua, maji, jotoridi, kuhakikisha mikakati ya kikanda na kimataifa ya nishati inatekelezeka kwa wakati, kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kufanya marekebisho ya sera na miongozo kwa wawekezaji wa sekta binafsi ili wawekeze katika sekta ya nishati. 



(Picha kwa hisani ya TBC)


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • ANUANI ZA MAKAZI KUJA NA FURSA LUKUKI ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

    May 26, 2025
  • WANAFUNZI NI SALAMA CHINI YA MRADI WA SHULE BORA .

    May 26, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.