• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

BALOZI WA IRELAND ATEMBELEA SINGIDA NA KUAHIDI KUSAIDIA UJENZI WA MABWAWA.

Posted on: September 15th, 2017

  Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock leo amefanya ziara mkoani Singida na kuahidi kuangalia namna ya kufadhili ujenzi wa mabwawa ili yaweze kusaidia kilimo cha umwagiliaji na sio kutegemea mvua pekee.

Mhe. Sherlock amewatembelea wanufaika wa misaada wanayotoa katika Vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi vya Siuyu na Faraja, mara baada ya yeye na mabalozi wengine kumaliza shughuli maalumu bungeni Dodoma.

Ameeleza kuwa amefurahishwa na hali ya hewa ya Mkoa wa Singida huku akisema kuwa uwepo wa barabara nzuri umerahisisha safari yake Mkoani hapa ambapo ni jirani na makao makuu ya nchi.

Mhe. Sherlock ameongeza kuwa anautazama mkoa wa Singida katika sura ya maendeleo zaidi kutokana na fursa zilizopo huku akiahidi kuanzisha miradi itakayosaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la alizeti linalozalishwa kwa wingi Singida.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema ameupokea ujio wa balozi huyo kwa furaha kubwa kwakuwa hiyo ni ishara ya kufunguliwa zaidi kwa milango ya mahusiano mazuri.

Dkt Nchimbi amesema moja ya faida ya Singida kuwa jirani na makao makuu ni kupata wageni ambao wanaitazama Singida kwa mtazamo wa maendeleo zaidi na ishara Singida itapata mabadiliko makubwa ya kiuchumi.

Amesema kilimo cha umwagiliaji kina tija zaidi kuliko kutegemea mvua pekee ambapo Singida inajipanga kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula nchini huku ikiwa na lengo la kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya makao makuu ya nchi ambayo maeneo mengi yatakuwa na shughuli za kiofisi zaidi.

Dkt Nchimbi amesisitiza Mkoa wa Singida hauna njaa, sio masikini na wala sio kame na wananchi wa singida wamejipanga kutumia fursa zozote zinazojitokeza kwa ajili la kukuza uchumi.

Aidha amewataka wananchi wa Singida kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuwa washiriki wakubwa katika kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda.


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KILIMO CHA MASHAMBA YA PAMOJA YA KOROSHO, WILAYA YA MANYONI – SINGIDA May 02, 2022
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • SINGIDA INVESTMENT GUIDE February 23, 2021
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2022 - MKOA WA SINGIDA December 24, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA: TUTAJENGA HOJA HOSPITARI YA MAKIUNGU IPANDISHWE HADHI KUWA HOSPITALI YA RUFAA

    August 18, 2022
  • TOENI USHIRIKIANO KWA MAKARANI WA SENSA WAKATI WA KUHESABIWA.- RC SERUKAMBA

    August 17, 2022
  • RC Serukamba, amewataka Makarani na Wasimamizi wa SENSA mkoani hapa kutanguliza uzalendo katika zoezi la SENSA

    August 16, 2022
  • SERIKALI Mkoa wa Singida imetenga Sh.Milioni 342.8 kwa ajili ya kutengeneza shughuli za lishe ambapo ni sawa na Sh. 1,239 kwa kila mtoto wa chini ya miaka mitano

    August 16, 2022
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida. Haki Zote Zimehifadhiwa.