• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

**CHANJO YA POLIO KWA NJIA YA SINDANO YAZINDULIWA SINGIDA**

Posted on: April 8th, 2025

Mkoa wa Singida umeungana na Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika utekelezaji wa zoezi la kitaifa la utoaji wa dozi ya pili ya chanjo ya polio kwa njia ya sindano kwa watoto chini ya miaka mitano, ikiwa ni jitihada za kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa huo hatari unaoweza kusababisha ulemavu wa kudumu au kifo.

Zoezi hilo limezinduliwa kupitia kikao kazi cha Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, kikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Halima Dendego kikijumuisha wataalamu wa afya, viongozi wa kisiasa na kidini, pamoja na maofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo walioeleza kwa kina umuhimu wa kampeni hiyo ya kitaifa.

       Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amewataka viongozi wa dini na kisiasa kutumia nafasi zao kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hiyo ili kufanikisha kampeni hiyo na kulinda afya ya watoto. Aidha, aliiomba Wizara ya Afya kutumia maabara za ndani ya nchi badala ya kutuma sampuli nje, akisema hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mhe. Maltha Mlata, amesema ni muhimu kuwapa wazazi na watoto elimu ya kutosha kabla ya kupewa chanjo ili kupunguza hofu. Pia amewahimiza viongozi wa afya kushirikiana na waganga wa jadi ambao mara nyingine huathiri mitazamo ya wananchi kuhusu chanjo.

Akizungumza na wajumbe wa kikao hicho, Mwezeshaji wa Kitaifa wa Chanjo ya Polio kutoka Wizara ya Afya, Bw. Bakari Hamad Bakari, amesema kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa dozi ya pili ya sindano ni kuongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya polio ambavyo bado ni tishio kwa watoto nchini Tanzania, hasa kutokana na mwingiliano wa watu kutoka mataifa yenye maambukizi. Alisema virusi vya polio vinaweza kuingia mwilini kupitia maji au chakula kilichochafuliwa, hukaa kwenye utumbo, kuongezeka kwa kasi na baadaye kuvamia mfumo wa fahamu na kusababisha kupooza.

Bw. Bakari ameeleza kuwa licha ya kuwa na chanjo ya awali ya matone, dozi ya pili ya sindano imeongezwa ili kuhakikisha watoto wanapata kinga ya kutosha, kwani watoto walio chini ya miaka mitano ndio waathirika wakuu wa polio. Amesisitiza kuwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa, kichwa kuuma, kutapika na kuhara, lakini mara nyingi mgonjwa hugundulika wakati tayari ameanza kupata ulemavu wa kupooza. Alionya kuwa mtoto yeyote chini ya miaka 15 anayepata kupooza ghafla bila sababu za ajali au kuumia ubongo, anapaswa kuchunguzwa kwa haraka kama mshukiwa wa polio.

Katika kikao hicho, baadhi ya wajumbe waliibua maswali kuhusu usalama wa chanjo na wito wa kuhakikisha elimu kuhusu huduma hiyo inaendelea kutolewa mara kwa mara ili kuondoa hofu miongoni mwa wazazi ambapo Mratibu wa Huduma ya Chanjo Mkoa wa Singida, Bw.Habibu Mwinory, aliwahakikishia wajumbe kuwa chanjo itatolewa katika vituo vya afya kwa utaratibu wa kawaida, bila kufanya kampeni mashuleni. Aliongeza kuwa watoto watakaopata madhara madogo baada ya chanjo watahudumiwa ipasavyo na wahudumu wa afya.


Bw. Bakari alihitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwa vituo vya afya endapo mtoto atapata dalili zozote za kushukiwa kuwa na polio, ili hatua zichukuliwe mapema. Alisisitiza pia umuhimu wa matumizi ya maji safi na salama, pamoja na kujenga utamaduni wa kupima afya badala ya kusubiri hali kuwa mbaya. Alisema kupima afya mapema ni hatua muhimu ya kuzuia madhara ya magonjwa sugu kama polio.

Kampeni ya utoaji wa dozi ya pili ya chanjo ya polio kwa njia ya sindano ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kuwa Tanzania inabaki salama dhidi ya maambukizi ya virusi vya polio, ikiwa ni hatua ya kuimarisha afya ya watoto na vizazi vijavyo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.