• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA SINGIDA MBIONI KUHAMIA MAJENGO MAPYA.

Posted on: September 23rd, 2025

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kampasi ya Singida, kimekamilisha ujenzi wa majengo  matatu katika awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho kwa gharama ya Shilingi 1,381,910,020.

Hayo yamejiri katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Chuo hicho Dkt.Emanuel Tandika katika ukaguzi na ufuatiliaji wa miradi uliofanyika siku ya leo Septemba 23,2025 katika Manispaa ya Singida ukiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga sambamba na timu ya ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 

Majengo yaliyojengwa katika awamu hii ni pamoja na majengo mawili ya madarasa na jengo moja la choo cha nje. Jengo la kwanza lina madarasa manne yenye uwezo wa kuchukua wanachuo 150 kila moja, ofisi sita, ukumbi mdogo mmoja na vyoo vya nje viwili. Jengo la pili lina madarasa manne yenye uwezo wa kuchukua wanachuo 90 kila moja, ofisi sita na ukumbi mdogo mmoja. Jengo la tatu ni choo cha nje chenye matundu tisa.

Awamu ya pili ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa majengo 30 katika kampasi hiyo. Majengo hayo ni pamoja na jengo la maabara ya kuchapia (typing laboratory), majengo ya madarasa, jengo la utawala, jengo la maktaba, ukumbi wa shughuli mbalimbali, ukumbi wa kisasa wa mikutano, zahanati, nyumba za wafanyakazi, maabara ya kompyuta, hosteli, jengo la mlezi wa wanachuo pamoja na jengo la mapumziko (rest house). Gharama ya jumla ya mradi mzima hadi kukamilika ni Shilingi 15,016,823,777.

  Katika taarifa ya maendeleo ya mradi huo iliyowasilishwa mbele ya timu ya ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Chuo kilieleza kuwa hatua inayofuata ni kuanza awamu nyingine ya ujenzi wa mabweni ya wanachuo. Hii inalenga kupunguza changamoto ya wanafunzi wengi kulazimika kuishi katika hosteli za watu binafsi kutokana na ukosefu wa mabweni ya kutosha.

Kadhalika uongozi wa Chuo pia umetoa wito kwa wawekezaji kujitokeza na kushiriki katika ujenzi wa hosteli kwa ajili ya wanachuo, kwa kuwa uhitaji wa huduma hiyo bado ni mkubwa.

Timu ya ukaguzi wa miradi kutoka Mkoa wa Singida iliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Daktari Fatuma Mganga, huku timu ya ufuatiliaji kutoka Manispaa ya Singida ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bi. Joanfaith Kataraia.




Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HALI YA HEWA YA MKOA WA SINGIDA YATAKIWA KUTUMIWA KAMA FURSA NA SIO KIKWAZO

    September 25, 2025
  • MRADI WA MABWAWA YA KUTIBU MAJITAKA KUKAMILIKA OKTOBA,WANANCHI KUNUFAIKA

    September 23, 2025
  • CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA SINGIDA MBIONI KUHAMIA MAJENGO MAPYA.

    September 23, 2025
  • "MSITUMIE NYUMBA ZA IBADA KUHAMASISHA VURUGU":RC DENDEGO

    September 21, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.