• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

DKT NCHIMBI APOKEA MADAWATI ZAIDI YA 2000 KUTOKA BUNGENI KWA NIABA YA MIKOA YA KASKAZINI.

Posted on: July 11th, 2017

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi leo ampokea madawati 2579 kutoka kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Akipokea madawati hayo yaliyosafirishwa katika magari 19 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Dkt Nchimbi amelipongeza jeshi hilo kwa uzalendo huo wa kuhakikisha mali za umma zinafika Singida kwa ajili ya kuanza kusambazwa katika halmashauri husika zikiwa salama na katika hali nzuri.

Dkt Nchimbi amelipongeza Bunge kwa uzalendo wa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka nchini  ili kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.

Amesema madawati hayo yataongeza motisha kwa wanafunzi kujisomea kwakuwa mazingira yatawawezesha kuandika na kusoma kwa ufanisi zaidi.

Aidha Dkt Nchimbi amezitaka halmashauri zitakazopokea madawati hayo kuhakikisha wanayatunza ili yadumu na kuwanufaisha wanafunzi kwa muda unaostahili.

“Madawati na yenyewe yanahitaji ukarabati, sio kwakuwa mmepewa basi muyaache tu, hapana, ukiona ubao unalegea kidogo basi hakikisha unarekebisha na sio kuanza kusubiri waliotupatia ndo waturekebishie”, amesema na kuongeza kuwa

“Ili madawati haya yadumu waalimu na wanafunzi kwa pamoja wahakikishe wanayatunza vizuri, hasa walimu wasimamieni wanafunzi na muaelekeze namna ya kuyatunza kwakuwa hii ni mali yetu sote”, Amesisitiza.

Aidha Dkt Nchimbi ameongeza kuwa mkoa wa Singida uko tayari kupokea vifaa na mambo mbalimbali ya kitaifa kutokana na kuwa katikati mwa Tanzania hivyo kuwezesha usambazaji kwa mikoa mingine kuwa rahisi.

“Tunakaribisha taasisi, mashirika, na hata serikali kuu kama kuna vifaa vingine leteni Singida ni katikati na usambazaji utakuwa ni rahisi, lakini pia hata shughuli zozote za kitaifa mkoa wa Singida uko tayari kabisa kuzipokea” amesema Dkt Nchimbi.

Kwa upande wake Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa  halmashauri ya Wilaya ya Meru Frank Paul Mwambachi amelishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kuwapatia madawati ambapo halmashauri yake imepata madawati 400.

Mwambachi amelishukuru  JWTZ kwa kuyasogeza madawati jirani na halmashauri yake hivyo itakuwa rahisi na salama zaidi kwake kuyasafirisha na kuyafikisha yakiwa katika hali nzuri na kwa uharaka zaidi.

“Madawati 400 wakikaa wanafunzi watatu watatu ina maana ni wanafunzi 1200 wamenufaika, kwakweli tunalishukuru sana bunge kwa uzalendo wao, pia jeshi limetusaidia sana kuyaleta madawati yetu Singida ambapo ni jirani” amesema Mwambachi.

Aidha ameongeza kuwa madawati hayo yataboresha mazingira ya ufundishaji na ya kujifunzia hivyo halmashauri itahakikisha wanayatunza ili wanafunzi wanufaike kwa kipindi kirefu.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.