• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF.

Posted on: December 9th, 2017

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameshauri Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) uanzishe kazi za ajira za muda kwa walengwa wa Mpango huo kutoka jamii ya Wahadzabe waliopo Wilayani Mkalama ili uwasaidie kuinua uchumi wao.

Dkt Nchimbi ametoa ushauri huo mara baada ya kutembela kijiji cha Singa Wilayani Mkalama na kuona bwawa litakalotumika kuhifandhi maji ya mvua kwa ajili ya shughuli mbalimbali lililojengwa na walengwa wa Tasaf Kijijini hapo kisha kutembelea kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza Wilayani  humo aliposhuhudia malipo ya walengwa wa kihadzabe wa Mpango wa Tasaf.

Ameeleza kuwa jamii ya wahadzabe hawana mradi unaohusisha kazi za ajira za muda ambazo zimekuwa zikisaidia katika kuongeza kipato, kuwafundisha thamani ya kazi pamoja na kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikisaidia jamii nzima kama vile mabwawa na  barabara.

“Nashauri TASAF kabla ya msimu huu wa mvua kuisha muwaletee na hawa wahadzabe mradi wa ajira za muda kama ambavyo walengwa wa vijiji vingine wamekuwa wakifanya kazi hizo na zimekuwa zikichangia maendeleo kwa vijiji vyao”, ameeleza na kuongeza kuwa,

“Miradi ya ajira za muda zitawafundisha Wahadzabe kujituma kufanya kazi ambazo zinachangia maendeleo ya jamii huku kazi hizi zikiwa kama darasa la wao kujifunza kwa vitendo kuwa kama anaweza kwa mfano kushiriki kujenga bwawa basi anaweza kufanya jambo kubwa katika familia au maisha yake”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Aidha ametoa tahadhari kwa walengwa hao wa kihadzabe kuwa wasitumie pesa wanayopewa kwa kunywa pombe badala yake pesa hiyo itumike sawasawa na maelekezo ya mpango huo na hatua zichukuliwe kwa wale watakaokaidi.

Kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji Kutoka Tasaf Makao Makuu Anna Njau ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa Dkt Nchimbi katika ziara yake ameeleza kuwa ushauri huo ni mzuri na una lengo la kuwasaidia wananchi kama ambavyo Tasaf imekuwa na lengo la kuinua jamii hasa kaya masikini hivyo wazo hilo ataliwasilisha makao makuu kwa ajili ya utekelezaji.

Baadhi ya wahadzabe waliofika kupokea fedha za Mpango wa Tasaf wameeleza kuwa fedha hizo zimewasaidia kuwainua kiuchumi kwa kuhakikisha wana chakula cha kutosha, watoto wameenda shule, watoto wadogo wamepelekwa kliniki huku wakijiendeleza zaidi kiuchumi kwa ufugaji mdogo wa kuku na mbuzi pamoja na kuboresha makazi yao.

Jamii ya Wahadzabe waliopo Kijiji cha Munguli na hasa kitongoji cha Kipamba Wilayani Mkalama wamekuwa wakiishi kwa kutegemea uwindaji wa wanyama pori, kula asali, ubuyu, matunda na mizizi mbalimbali ambapo juhudi za Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf) umesaidia jamii hiyo kuanza kupeleka watoto shule, kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na ufugaji.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.