• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Fungeni Mifumo Ya Kamera Ya Usalama Katika Majiji Makubwa – Waziri Mkuu

Posted on: August 30th, 2021

Wizara ya mambo ya ndani imetakiwa kukamilisha kwa haraka mikakati ya ufungaji wa mifumo ya kamera za usalama katika majiji makubwa hapa nchini yakiwemo Dar es salaam Dodoma, Mbeya Tanga Arusha na Mwanza kwa kuwa  mifumo hiyo itatumika kufuatilia mienendo ya watu ambao wenye nia ya kuvuruga amani na usalama katika maeneo hayo.

Pia Wizara hiyo imetakakiwa kuendelea kujenga miudombinu na makazi ya askari polisi na magereza ili kuboresha mazingira yao  ya kufanyia kazi  ambayo  yanaongeza chachu katika kuimarisha ulinzi wa Raia na mali zao.

Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa (Mb) ameyasema  hayo leo tarehe 30.08.2021 wakati wa ziara yake mkoani Singida ambapo alizindua majengo mawili ya ofisi za Kamanda  wa Polisi  na  ofisi ya mkuu wa Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani humo.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu amempongeza IGP Sirro kwa usimamizi mzuri wa majengo hayo ambapo Jengo la ofisi ya Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia limegharimu kiasi cha milioni 499  na jengo la mkuu wa polisi mkoa wa Singida limegharimu  shilingi 469.4

 Aidha katika ziara hiyo Waziri Mkuu amelitaka Jeshi la Polisi nchin kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassani  kusimamia haki  na kuhakikisha wanapunguza matumizi ya nguvu  kupita kiasi kwa Raia.

Hata hivyo Waziri Mkuu amelitaka Jeshi hilo kutumia wasanii  na vipeperushi kwa kupeleka  elimu kwa jamii ili kuwashirikisha katika masuala ya ulizi na usalama pamoja na kuimarisha madawati ya jinsia kwa kila eneo ili kupunguza dhana za uhalifu katika jamii.

Aidha Waziri Mkuu amewataka kushirikisha vyombo mbalimbali vya sheria ili kusaidia kupunguza mlundikano wa kesi na mahabusu hapa nchini.

Kwa upande wake IGP SIRO amesema Ujenzi wa majengo haya mawili  umekamilishwa tarehe 15/07/2021 kwa gharama ya Tshs 1,314,299,300. kwa majengo yote mawili. 

Jengo la ofisi ya Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia likiwa na jumla ya vyumba vya ofisi 14 na linatosheleza mahitaji.

Aidha jeshi la polisi limejiwekea mkakati wa  kutoa elimu kwa wananchi kuliamini Jeshi lao na kuwafichua Wahalifu na Uhalifu pamoja na kushirikiana kwa karibu na wananchi, viongozi wetu wa Vitongoji, Vijiji, Mitaa, Kata, Tarafa, Wakurugenzi, Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya, Mikoa hadi Taifa katika kutekeleza mikakati ya ulinzi na usalama kwenye maeneo yetu.

IGP Sirro amesema tayari watekeleza mpango wao wa  Kupunguza mlundikano wa Mahabusu kwenye vituo vya Polisi na   Mahabusu Magerezani kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya Sheria hususani Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali – DPP na Jeshi la Magereza. 

Aidha IGP  amemhakikishia waziri mkuu kwamba Jeshi la Polisi mkoani Singida litaendelea kujenga na kuboresha miundo mbinu ya majengo ya Jeshi la Polisi nchini hatua kwa hatua kulingana na upatikanaji wa fedha kwa lengo la kuwajengea mazingira mazuri ya kazi Maafisa, Wakaguzi, Askari na Watumishi Raia.

Awali RC Singida Dkt. Binelith Mahenge amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara, madaraja, ujenzi wa shule na umeme ambapo kila wilaya kuna miradi mbalimbali inaendelea

Amesema katika wilaya ya Mkalama kuna mradi wa ujenzi wa madarasa unaendelea lakini kuna ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya, daraja linalounganisha mkoa wa Simiyu na Singida .

Hata hivyo RC ameeleza uwepo wa changamoto ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya  Ikungi na kumuomba Waziri mkuu aweze kuona namna ya kusaidia kwenye utatuzi wa changamoto hiyo.

Mwisho

Imeandaliwa na

Ofisi ya RC- Singida .

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.