• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

HALMASHAURI SABA ZA MKOA WA SINGIDA ZAVUNJA REKODI UKUSANYAJI MAPATO, SERIKALI YA MKOA YAPONGEZA.

Posted on: July 30th, 2024

Halmashauri Saba za Mkoa wa Singida zimevuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka asilimia 90 kwa miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia 101 kwa kukusanya Bilioni 21.32 kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Halmashauri hizo ni Ikungi, Mkalama, Singida, Iramba, Manyoni, Itigi na Manispaa ya Singida.

Katika Hotuba yake ya kufungua Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) ambapo angenda lengwa ikiwa ni Ukusanyaji Maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 mkoa wa Singida, Mkuu wa mkoa huo Mheshimiwa Halima Dendego, amesema malengo hayo yamefikiwa kutokana na mipango na mikakati madhubuti ikiwemo uanzishaji wa vyanzo vipya vya mapato na ushirikiano mzuri kati ya Watendaji na Viongozi wao.

“Nawapongeza kwa hatua hizi mlizochukua kwa kuvuka malengo katika ukusanyaji wa mapato ongezeni bidii zaidi katika ukusanyaji, Amesisitiza Dendego.

Dendego pia amezipongeza Halmashauri za mkoa wa Singida kwa kupata hati safi katika ukaguzi.

Kuhusu fedha za Miradi ya Maendeleo, Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ameishukuru Serikali Kuu kwa kuupatia mkoa wa Singida Bilioni 241 sawa na asilimia 105 hadi kufikia Juni mwaka huu kwa ajili ya shughuli za utawala na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amevunja rekodi ya kuupatia mkoa wa Singida fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikilinganishwa na miaka mingine ambapo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 mkoa iliidhinishiwa zaidi ya Bilioni 230 lakini umepewa fedha zaidi ya bilioni 241 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Sijawahi kuona katika miaka yangu ya Uongozi kwa Serikali kutoa fedha zaidi ya tulizoomba lakini kwa Rais Samia hili limewezekana Tunamshukuru Sana tena sana,” Amesisitiza Dendego.

Kuhusu miradi ya Umwagiliaji, Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amesema Serikali inaendelea kukarabati na kujenga miradi mipya ya umwagiliaji ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Amesema kwa sasa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umwagiliaji inaendelea vizuri ukiwemo mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkalama na Msange katika Halmashauri ya wilaya ya Singida kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 55.

Dendego ameeleza kuwa miradi hiyo Miwili ya umwagiliaji ikikamilika itaufanya mkoa wa Singida kuwa na hekta 4000 za umwagiliaji hali ambayo itaongeza maradufu shughuli za uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga akizungumza kwenye kikao cha kusanyaji Maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 mkoa wa Singida.

Kikao cha ukusanyaji wa maoni kuhusu dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kikiendelea.



Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.