Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Singida kwa usimamizi wa Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea mkoani humo hivi sasa.Waziri Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea kukagua ujenzi wa kituo cha afya Kintinku kilichopo wilayani Manyoni mkoani Singida. Waziri Jafo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho serikali imepeleka sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.Amebainisha Mkoa wa Singida unaendelea ujenzi katika vituo saba ambapo kila eneo maendeleo ya ujenzi yanaenda vyema.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Manyoni mashariki Daniel Mtuka kwa juhudi zake za kuwahangaikiwa wananchi wa Jimbo hilo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.