• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Jopo la Mawaziri Wanane na Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Kisekta wakutana mkoani Singida kutathimini na kupendekeza namna ya kumaliza migogoro ya Ardhi

Posted on: October 8th, 2021

Jopo la Mawaziri Wanane na makatibu wakuu kutoka wizara za kisekta  wametembelea vijiji Kumi na mbili (12)  mkoani Singida vyenye migogoro ya ardhi ili  kutathimini na kupendekeza namna ya kumaliza migogoro hiyo.

Akiongea leo tarehe 8 Oct. 2021 wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa mkuu wa Mkoa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi amesema  Timu hiyo iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano itatembelea vijiji 920 vyenye migogoro ya ardhi katika Mikoa 10  ambapo 12 na viwili vipo mkoani Singida.

Amesema lengo la timu hiyo ni kuhakikisha wanatatua migogoro hiyo iliyoripotiwa awali na kuhakikisha inakwisha pasipo kuleta taharuki ambapo pia mipaka itawekwa ili kuwasaidia wananchi.

Amesema katika migogoro ya ardhi au ile ya  wakulima na wafugaji imekubalika na Baraza la Mawaziri kwamba Muungano huo wa wizara za kisekta ndio utakao tumika kutatua migogoro ya namna hiyo badala kila wizara kwenda yenyewe.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akishukuru timu hiyo amesema Mkoa utatoa ushirikiano kuhakikisha tathmini hiyo inakamilika na wananchi wanaendelea kuishi katika maeneo hayo.

Amesema maeneo yenye migogoro ya ardhi ni Wilaya ya Iramba, Singida, Ikungi na Manyoni na kuomba maeneo ambayo yana mgogoro na baina ya Jeshi na wananchi na ambayo Jeshi haliyatumii  busara zitumike wapewe wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge alisema, Ofisi yake sasa itahakikisha inasimamia pamoja na kuifatialia migogoro yote ya ardhi ikiwemo ile ya mipaka katika wilaya na vijiji ili kumaliza kabisa migogoro ya ardhi.

Wakiwa katika Manispaa ya Singida Mawaziri hao wametembelea eneo la Mwankoko lenye mgogoro ulioanza mwaka 2016 kati ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini hapa (SUWASA) na wananchi wanaolalamikia kupunjwa fidia waliyolipwa na Serikali ili kupisha utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Mwankoko ambapo baada ya Mawaziri kusikiliza pande zote mbili, Mwenyekiti wa Kamati wa Mawaziri wa Kisekta ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amemwagiza Mthamini Mkuu wa Serikali kufika mkoani hapa siku ya Jumatatu tarehe 11 Oct. 2021 ili kufanya uchunguzi na kujua ukweli kuhusu malalamiko hayo.

Mawaziri hao wa kisekta waliokuwa kwenye ziara hiyo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TAMISEMI, Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mazingira, Utalii, Ulinzi na Maji.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.