• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Katatueni kero za wananchi vijijini – Waziri Mkuu

Posted on: July 16th, 2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Halmashauri ya Iramba kuwafuata wananchi vijijini ili kuwasikiliza na kutatua kero zao badala ya kuwasubiri wananchi maofisini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika Kata ya  Mtoa Wilayani hapo wakati wa  kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya cha Mtoa  kilicho gharimu Tsh. Milioni 662

Amesema  kwa jographia ya Wilaya ya Iramba  vijiji vipo mbali na ofisi za Serikali jambo ambalo inawagharimu fedha nyingi kufika kwenye ofisi hizo kupata huduma.

"Leo mimi nimetoka ofsini kwangu nimekuja Kata ya Mtoa kutatua kero za Wananchi sasa na nyie watumishi wa umma mtoke ofsini mkawahudumie wananchi huko walipo" Alisema

Aidha amewataka watumishi kuwa waaminifu na kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kutumia utaalamu wao kuleta matokeo chanya.

Amesema watumishi wahakikishe wanawasikiliza wananchi na wasiwafukuze maofisini badala yake waende Vijijini kuwaeleza fursa ambazo zinatekelezwa na Idara mbalimbali kama Afya na kilimo.

"Shirikianeni na Madiwani kuwafikia wananchi na waelezeeni mafanikio ya Serikali, nendeni kwa wananchi mkawape huduma na kusikiza kero zao".

Waziri Mkuu akaendelea kusema kwamba kumekuwepo na changamoto ya usimamizi  wa vyanzo vya mapato hivyo kusababisha upotevu na hasara kwa Serikali hivyo kuwataka wakuu wa Idara kutekeleza majukumu yao na kila Idara ihakikishe inafanya kazi yake ili kuleta mabadiliko.

Waziri Mkuu amewataka Maafisa Tawala wa Wilaya kuhakikisha kwamba watumishi wanatekeleza majukumu yao na wanakuwa na maadili ndani ya Halmashauri na kuwachukulia hatua wote watakaokwenda kinyume.

Katika hatua nyingine ameeleza kuhusu utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kulinda miradi ya maji ambayo Serikali imetumia fedha nyingi kuitengeneza.

Waziri Mkuu amezitaka kamati za maji na Mazingira kusimamia vyanzo vya maji na kuzuia uharibifu wa  Mazingira ili kuongeza upatikanaji wa maji kama ilivyokuwa awali.

Aidha amesema awali maji yalikuwa yakitiririka maeneo mengi katika Kata hiyo lakini kwa sababu mifugo imekuwa ikiingizwa katika vyanzo vya maji na kwenye hifadhi za mazingira.

Amesema Misigiri imekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu  lakini changamoto hiyo itakwisha  kwa kuwa mradi wa maji umekamilika hivyo kila nyumba utapata maji alisisitiza Waziri Mkuu.

Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Serikali imetenga Bilioni 5.1 kwa aji ya miradi ya maji katika Wilaya ya Iramba ikiwa ni pamoja na mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria aliendelea kueleza Waziri Mkuu.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.