• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025,TAKUKURU SINGIDA WATOA SOMO

Posted on: February 11th, 2025

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Singida leo Februari 11,2025 wametoa elimu kwa viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa kimila,wazee maarufu,viongozi wa asasi zisizo za kiserikali na watu wenye mahitaji maalumu juu ya madhara ya rushwa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu 2025,mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi(NAO)mkoani Singida.


Awali akiwasilisha mada katika semina hiyo,Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU mkoani Singida, Bw.Joseph John Kailanya ametoa mada kuhusu aina za rushwa katika uchaguzi,makosa ya jinai katika katika uchaguzi na njia mbali mbali za kuripoti taarifa za vitendo vya rushwa na madhara ya rushwa.

"Baadhi ya makosa ya jinai katika uchaguzi ni pale mgombea alijitoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kwa kupewa rushwa,kuandaa makundi ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi,Mpigakura kumpatia mtu mwingine kadi ya mpiga kura ili kuitumia na kutoa shukurani kwa wapiga kura baada ya uchaguzi kufanyika"amesema Bw.Joseph Kailanya.

Naye Mkuu wa TAKUKURU mkoani Singida Bi.Sipha  Mwanjala akizungumza katika semina hiyo ameainisha majukumu ya Taasisi hiyo ambayo ni "KUZUIA NA KUPAMBANA"na rushwa kwa lengo la kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mmoja.Pia amewasisitiza wananchi kutumia jukwaa la 'TAKUKURU RAFIKI' ili kupata elimu kuhusu Masula ya rushwa na pia kuwawezesha kuibua kero mbalimbali na kupendekeza namna gani ya kuzitatua.

Pia amewaasa viongozi wa dini kwenda kuelimisha waumini wao kuhusu suala la rushwa kama kosa la kijani na adui mkubwa sana wa kupata viongozi bora na waleta maendeleo.

Akitoa maoni katika semina hiyo,Chifu Mazoya ameomba taasisi hiyo kupeleka elimu hiyo ya rushwa katika makundi na sehemu mbalimbali ili watubwafahamu zaidi kazi zao na kuwafahamisha tofauti ya taasisi hiyo na Askari wa  Polisi kwa madai kubwa wananchi wanachanganya majukumu ya taasisi hiyo na yale yanayofanywa na Askari wa Polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ambaye alikua mgeni rasmi katika semina hiyo amezungumzia kuhusu madhara ya rushwa katika uchaguzi akiainisha baadhi ya madhara yake hasi ikiwemo kuchagua viongozi wasiofaa katika jamii ambao hushindwa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi pamoja na kuharibu misingi ya demokrasia ambayo hupelekea kuharibu amani na uchumi wa jamii na nchi yetu kwa ujumla.

"Tunao wajibu wa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuiepuka rushwa hususani katika kipindi kijacho cha uchaguzi,ili kuwapata viongozi bora ni lazima tuikemee rushwa ili kudumisha haki na uwajibikaji wao kwa wananchi"amesema Mhe.Dendego.

Pia ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa TAKUKURU kwa wakati wowote watakapohitaji ushirikiano wao,pia kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatosha kwa lengo la kuhakikisha utendaji bora wa kazi na kwa haki kwa kuhakikisha wote watakaohusika katika vitendo hivyo wanachukuliwa hatua za kisheria.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.