• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

KUKU FESTIVAL MEI MOSI SINGIDA MAANDALIZI YAMEKAMILIKA

Posted on: April 2nd, 2025

Mkuu  wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, amewataka wafanyabiashara wanaochoma nyama ya kuku mjini Singida kujipanga kwa ajili ya kutoa huduma hiyo vizuri kwa mamia ya wageni ambao watakuja  kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (Mei Mosi) ambayo yatafanyika kitaifa mkoani hapa.

Alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza saa 3:00 usiku akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mheshimiwa Godwin Gondwe, Meya wa Manispaa ya Singida Mhe.Yagi Kiaratu, Katibu Tawala Wilaya ya Singida, Bi.Naima Chondo katika eneo la Ubungo Singida mjini ambalo ni maalum kwa ajili ya wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuchoma nyama ya kuku kwa saa 24.

"Tumekuja kuwatembelea hapa kuona hali ilivyo hapa ili wageni wetu watakaokuja kwa ajili ya Mei Mosi wasijisikie vibaya, tunategemea zaidi ya wageni 6000 katika mjini wetu wa Singida na wote wataishi hapa Manispaa ya huduma zote wanategemea kuzipata hapa hapa,"alisema.

Mhe.Dendego amesema kutokana na ugeni huo mkubwa kila mfanyabiashara ajipange kwa kuhakikisha anatoa huduma nzuri na katika mazingira safi ili hata watakapokuwa wameondoka wasimulia jinsi kuku wa Singida walivyo wazuri na watamu.

Naye Meya wa Manispaa wa Singida, Yagi Kiaratu, alishukru kwa mkoa wa Singida kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa siku ya Mei Mosi kwani hali hii itaweza kuongeza kipato kwa wananchi wa Manispaa ya Singida ambao watatumia fursa hiyo kufanya biashara mbalimbali.

"Singida ni mkoa ambao vyakula vya asili vinapatikana, hapa wageni wetu wakija watakula kuku wa asili, ng'ombe wa asili wageni watafurahia vyakula vizuri na vitamu na sisi tumejipanga kutoa huduma kwa kukesha hadi asubuhi," alisema.

Naye Katibu wa Wafanyabiashara Wachoma Kuku eneo la Ubungo, Joseph Raphael, aliishukru serikali kwa kuileta Mei Mosi kitaifa Singida na kwamba wamejipanga kutoa huduma nzuri za nyama ya kuku.

Alisema changamoto zilizopo katika eneo hilo watahakikisha wanazimaliza ili wageni wakija waweze kupata huduma nzuri za chakula na kwamba kwa sasa wameanza kutumia nishati safi ya gesi ili kuweza kuwahudumia kwa uharaka zaidi.

Kabla ya kilele cha maadhimisho ya Mei Mosi shughuli mbalimbali zitafanyika kama vile michezo,utalii wa barabarani lengo likiwa kuwaonyesha wageni wataofika Singida wajue Singida kuna utalii gani.

Sambamba na maandalizi hayo,Mei Mosi Mkoani Singida linatarajiwa kuwa na usiku wa Kuku ( kuku festival), mashindano ya magari, ngoma za asili, makongamano na bonanza la michezo litakaloanza wiki mbili kabla ya kilele cha Mei Mosi.


               "KARIBU SINGIDA-MEI MOSI 2025.' 

                          SINGIDA NI SALAMA

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.