• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MAJARIBIO YA MBEGU CHOTARA YATOA MATUMAINI MAPYA KWA WAKULIMA NA WASINDIKAJI WA ALIZETI SINGIDA.

Posted on: November 19th, 2017

  Wakulima na wasindikaji wa zao la Alizeti Mkoani Singida wameonekana kufurahia na kupata matumaini mapya mara baada ya kushuhudia matokea ya majaribio ya usindikaji wa mbegu chotara ya Alizeti mkoani Singida.

Wakulima na wasindikaji hao wameshuhudia majaribio ya usindikaji wa mbegu chotara ya alizeti yakifanyika katika kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti cha Nuru mjini Singida, kwa kukamua mbegu chotara na zile za zamani kisha kulinganisha kiwango cha mafuta na mashudu yaliyopatikana.

Mbegu chotara zilizofanyiwa majaribio zimepandwa na wakulima mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya majaribio hayo, ambapo matokeo yameonyesha kuwa mbegu chotara zinatoa mazao mengi, mafuta na mashudu mengi, zinatumia muda kidogo shambani mpaka kuvunwa, zinatumia maji kidogo na hazishambuliwi na magonjwa ikilinganishwa na mbegu za zamani.

Mmoja kati ya wakulima aliyeshiriki majaribio ya kulima mbegu hizo Kutoka Ihanja Wilayani Singida John Thomasi alihudhuria pia majaribio ya usindikaji wa mbegu hizo na kusema kuwa sasa wakulima wa alizeti wamepata mwanga kwa kuona namna ambavyo kilimo cha alizeti kwa kutumia mbegu chotara ya alizeti kitawakomboa.

“Mimi ni mmoja kati ya waliolima hizo mbegu chotara kama sehemu ya majaribio na tuliona kwa kuanzia shambani hazisumbui, zinatumia maji kidogo, na mavuno ni mengi, kilichobaki ilikuwa ni kujua ubora wake katika kutoa mafuta na mashudu jambo ambalo tumeshuhudia leo kuwa mbegu hizi zinatoa mafuta mengi kuliko zile za zamani”, amesema Thomasi

Meneja Msimamizi Maarifa na Mawasiliano kutoka shirika la AMDT Al-amani Mutarubukwa amesema shirika hilo linalojikita katika Kilimo cha alizeti nchini hasa katika kuboresha mfumo wa masoko, uzalishaji na usindikaji lilifanya utafiti ulioonyesha kuwa changamoto kubwa ya wakulima wa alizeti ni kutokuwa na mbegu bora.

Mutaburukwa amesema kwakuwa mbegu zilizokuepo zimekuwa hazitoi mazao ya kutosha Shirika hilo lilifadhili majaribio ya mbegu chotara Mkoani Singida kupitia mradi wa Faida Market link kwa kuwezesha wakulima kupanda mbegu hizo.

Ameongeza kuwa matokeo ya majaribio hayo yamekuwa mazuri ambapo kwa upande wa mavuno mbegu chotara zimethibitika kutoa mazao mengi ambapo kwa ekari moja mkulima mmoja ameweza kuvuna gunia 16 ambapo kwa mbegu za zamani angeweza kuvuna gunia 3 mpaka tano.

Mutaburukwa amesema “Mara baada ya kuvunwa kwa alizeti hiyo AMDT pia imefanya majaribio ya kusindika mbegu hizo ambapo kilogram ishirini za mbegu chotara zimetoa mafuta lita sita ambapo mbegu za zamani zimetoa lita tano kwa kilo hizo hizo, huku mashudu yakipatikana kilogram 14 kwa mbegu chotara tofauti na kilogram 13 za mbegu za zamani.

Ameongeza kuwa Sifa ya mbegu hizo chotara ni kutoa mazao mengi, kutumia maji kwa ufanisi, zinastawi katika udongo wa aina zote, na pia hazikai shambani mda mrefu kabla ya kuvunwa ambapo hutumia siku 84 mpaka kuvuna tofauti na siku 97 kwa mbegu za zamani.

Naye Mwakilishi wa Meneja wa Faida Mali Mary Daniel amesema majaribio ya mbegu chotara yalianza mwenzi wa nne na yalihusisha halmashauri nne ambazo ni Mkalama, iramba, ikungi na Singida, ambapo mbegu ziliyotumika katika kufanya majaribio ya usindikaji zililimwa Kijiji cha ihanja wilaya ya ikungi.

Mary amesema wakulima waliofika kushuhudia majaribio ni 25 na wasindikaji 12 kutoka katika wilaya ya singida na ikungi ambao kwa pamoja wameazimia kutumia mbegu ya chotara na kuwaelimisha wakulima wenzao faida ya mbegu hizo.

Ameongeza kuwa makampuni mawili ya SDC na BYTRADE wamejiandaa kusambaza mbegu chotara kwa wakulima wa mkoa wa Singida huku akiwahakikishia wakulima kuwa wasambazaji hao wataleta mbegu kwa wakati ili wapande ndani ya msimu wa kilimo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.