• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MARUFUKU SHULE MKOANI SINGIDA KUNUNUA CHAKI NJE YA MKOA; RC NCHIMBI.

Posted on: September 26th, 2017

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa.

Dkt Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na  ikiwa haijapata soko.

“Hawa wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza kuwa,

“Yani mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”.

Dkt Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa kuunga mkono viwanda hivyo.

Amezitaka halmashauri kushirikiana katika kuboresha mazingira ya utendaji wa viwanda hivyo hasa kwa kuangalia namna ya kuboresha barabara zinazoenda katika machimbo ya jasi yanayotumika kutengeneza chaki kwakuwa wenye viwanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hizo.

Aidha Dkt Nchimbi ametoa wito kwa wenye viwanda wote nchini ambao wanatumia madini ya jasi (gypsum) katika shughuli zao wasihangaike kutafuta madini hayo bali waje singida kuna viwanda vinatengeneza madini hayo kwa ubora mzuri na bei nzuri.

Amesema viwanda vya kutengeneza jasi Singida vimekuwa vikizalisha madini hayo kwa wingi hivyo wenye uhitaji wa madini hayo kutengenezea chaki, gypusum board POP, wanakaribishwa kununua madini hayo mkoani hapa.

Dkt Nchimbi amewapongeza wenye viwanda hivyo kwa kutumia rasilimali kama madini ya jasi iliyopo Singida kwa kuanzisha viwanda mabavyo vinatengeneza ajira na kukuza uchumi kwa kuwa wao wamekuwa walipa kodi wazuri.

Naye Meneja wa kiwanda cha chaki cha Dober Color kilichopo Itigi Abdul Mahamoud amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hatua yake ya kukataza kuagizwa chaki nje ya Singida kwakuwa kutaongeza soko ambalo litasaidia viwanda hivyo kukua.

“Mkuu wa Mkoa tunashukuru kwa katazo hilo kwakuwa litafanya viwanda vyetu vikue na kuongeza uzalishaji, lakini pia itafanya viwanda hivi viongeze ajira na hata kodi tunayolipa itaongezeka hivyo kukuza uchumi wa Singida”, amesema Mahamoud.

Ameongeza kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinazalisha tani hamsini kwa siku lakini kutokana na katazo hilo matarajio ni kuongezeka uzalisha hadi kufikia tani 200 za chaki kwa siku.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.