• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MIRADI WILAYANI ITIGI KUNUFAISHA MAELFU YA WANANCHI.

Posted on: May 21st, 2025


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Ikungi leo Mei 21, 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujio wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa wilayani humo Julai 25, 2025.


Katika ziara hiyo, Mhe. Dendego ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga pamoja na viongozi wengine wa Kamati ya Usalama na Maendeleo ya Mkoa, ambapo walitembelea na kukagua utekelezaji wa miradi kadhaa inayogusa sekta za afya, maji, elimu, barabara, uvuvi pamoja na uwezeshaji wa vijana.


Ukaguzi huo ulianza katika mradi wa maji katika Kijiji cha Nsunsu, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, ambao ulianza kutekelezwa mwezi Mei 2024 na kukamilika Novemba 2024 kwa kutumia wataalamu kutoka RUWASA. Mradi huu umegharimu shilingi 415,993,640 na una uwezo wa kuhifadhi lita 50,000 za maji safi, ambapo unatarajiwa kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji jirani.


Aidha, Mkuu wa Mkoa na ujumbe wake walitembelea daraja la Konkilangi lenye urefu wa mita 50 lililojengwa katika barabara ya Shelui–Sekenke–Tulya–Tyegelo, sambamba na ujenzi wa barabara ya maingilio yenye urefu wa kilometa 1.5 kwa kiwango cha changarawe. Mradi huu unaogharimu kiasi cha shilingi 6,698,257,300 unatarajiwa kuimarisha mawasiliano ya Mkoa wa Singida na Ukanda wa Ziwa kupitia daraja la Mto Sibiti ambalo tayari limekamilika.


Katika sekta ya afya, walitembelea Zahanati mpya ya Mseko iliyopo Kata ya Mgongo, Tarafa ya Shelui, ambapo ujenzi unahusisha jengo la OPD na RCH, jengo la wazazi, nyumba ya watumishi, vyoo, kichomea taka, shimo la majivu, uzio pamoja na mnara wa maji. Mradi huu unakadiriwa kugharimu shilingi 250,000,000 na unatarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 3,337 pindi utakapoanza kutoa huduma rasmi.


Kwa upande wa elimu, walikagua ujenzi wa chumba kimoja cha darasa katika Shule ya Msingi Luono iliyopo Kata ya Kidaru, Tarafa ya Kisiriri, ambapo mradi huo unagharimu shilingi 23,000,000 kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri. Mradi huo unahusisha pia utengenezaji wa madawati 15, meza moja na kiti cha mwalimu kwa ajili ya wanafunzi 45.


Viongozi hao pia walitembelea ujenzi wa Shule mpya ya Awali na Msingi Yombo iliyopo katika Kijiji cha Tulya, Tarafa ya Kisiriri. Shule hiyo imejengwa kwa kujumuisha vyumba saba vya madarasa ya msingi, madarasa mawili ya elimu ya awali, matundu ya vyoo, kichomea taka, jengo la utawala, uzio wa madarasa ya awali na viwanja vya michezo. Mradi huo unatarajiwa kuwahudumia wanafunzi 272 wa elimu ya awali na 226 wa shule ya msingi, hivyo kuwaepusha kutembea umbali mrefu kufuata elimu, hususani kutoka vitongoji vya Yombo na Bambalaga.


Katika jitihada za kuwawezesha vijana kiuchumi, Mkuu wa Mkoa alitembelea kikundi cha vijana cha “NGUVU MOJA” kilichopo Kata ya Tyegelo ambacho kilipatiwa mkopo wa shilingi 7,000,000 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Mkopo huo uliwawezesha vijana hao kununua shamba la ekari nne kwa ajili ya kuweka mashine, kulipia eneo la kilimo cha mpunga ekari nne na kuendesha biashara ya kununua na kuuza mpunga. Baada ya mafanikio ya awamu ya kwanza ya mkopo, kikundi hicho sasa kimeomba mkopo wa awamu ya pili wa shilingi 22,000,000 kwa ajili ya kununua mashine ya kukoboa mpunga, kujenga jengo la kufunga mashine hiyo, pamoja na kuendeleza biashara ya mpunga na mchele.


Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mhe. Halima Dendego aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa hatua nzuri ya maandalizi ya miradi ya Mwenge wa Uhuru na kusisitiza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo uendelee kwa kasi na ubora unaokidhi thamani ya fedha za umma. Pia aliwataka wasimamizi wa miradi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati ili iweze kuzinduliwa, kuwekwa mawe ya msingi au kukaguliwa bila changamoto yoyote wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwezi Julai.


Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga alieleza kuwa ofisi yake itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote kwa kuhakikisha inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa, huku akisisitiza uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na usimamizi madhubuti.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MIRADI WILAYANI ITIGI KUNUFAISHA MAELFU YA WANANCHI.

    May 21, 2025
  • KAMATI YA USHAURI NA KLINIKI YA SHERIA YAZINDULIWA SINGIDA

    May 19, 2025
  • MAGARI MAPYA WILAYANI,UTENDAJI KUIMARIKA!

    May 19, 2025
  • SERIKALI KUU YAMWAGA FEDHA ZA MIRADI MANISPAA YA SINGIDA

    May 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.