Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Kerry William Silaa (Mb.) amehitimisha ziara yake ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo mkoani Singida, akizuru wilaya ya Ikungi. Akiwa huko, alizindua mradi wa maji katika kijiji cha Mnang’ana, uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 380 na utahudumia wakazi wapatao 3,000.
Waziri Silaa pia alizindua shule ya sekondari ya Puma, iliyogharimu milioni 106.4, ikijumuisha madarasa manne na matundu 8 ya vyoo na kuongeza uwezo wa kuchukua wanafunzi kutoka 80 hadi 160.
Aidha, alitembelea jengo la huduma ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Ikungi, ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya bilioni 2.7.
Ziara hiyo ilihitimishwa na mkutano na viongozi na watumishi wa mkoa, ambapo Waziri Silaa alimhakikishia Rais Samia kuwa fedha nyingi zimewezesha maendeleo makubwa katika mkoa huo.
#RAISSAMIANAMAENDELEOWASIKIENAWAONE #KaziIendelee
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.