• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

* RC DENDEGO ATOA WITO WA MABORESHO YA MAADILI NA TAALUMA

Posted on: April 10th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego,  amefungua rasmi Mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari wa Kanda ya Kati unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu (TIA), Singida, kuanzia tarehe 10 hadi 11 Aprili 2025, akitoa rai kwa walimu na viongozi wa shule kuhakikisha elimu inaimarishwa kwa misingi ya maadili, uzalendo na uwajibikaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo unaowakutanisha wakuu wa shule kutoka mikoa ya Singida na Dodoma, Mhe. Dendego ameeleza kuwa ni wakati wa kuwekeza nguvu kubwa katika kupambana na changamoto sugu zinazoikabili sekta ya elimu, hasa utoro wa wanafunzi, mimba za utotoni, na kushuka kwa maadili mashuleni.

“Lazima tushirikiane kuhakikisha tunalinda maadili ya vijana wetu. Wanafunzi wakilelewa vizuri shuleni, taifa linajenga msingi imara wa viongozi wa baadaye,” amesema.

Ameeleza kuwa mikutano ya aina hii ya kitaaluma ni muhimu kwa kuwa inatoa nafasi kwa wakuu wa shule kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto kwa pamoja na kutoa suluhisho zinazotekelezeka kwa lengo la kuinua ubora wa elimu nchini.

Aidha, aliupongeza umoja wa wakuu wa shule kupitia TAHOSA kwa kuendelea kushikamana, kusimamia maendeleo ya taaluma pamoja na kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya serikali, hususan ile ya miundombinu ya elimu inayotekelezwa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Nyie wakuu wa shule mmekuwa viongozi mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi ya elimu – mmekuwa wahandisi wa maendeleo. Hongereni sana kwa uzalendo na uaminifu,” alisema Dendego kwa msisitizo.

RC Dendego alitumia jukwaa hilo pia kuwakumbusha walimu kushiriki kikamilifu kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo mwaka huu yanafanyika kitaifa mkoani Singida, akisema hiyo ni fursa ya kipekee kwa walimu kuonesha mshikamano wao kama sehemu ya watumishi wa umma.

Kwa upande wao, viongozi wa TAHOSA walisema mkutano huo umeandaliwa kwa lengo la kuimarisha uratibu wa shughuli za kitaaluma na kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa serikalini kuhusu maboresho ya sekta ya elimu.

Mkutano huu wa siku mbili unaendelea kujadili mada mbalimbali zikiwemo za uongozi wa shule, malezi ya wanafunzi, usimamizi wa mitihani, matumizi ya TEHAMA katika kufundishia, na kuboresha mazingira ya kufundishia kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.