• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Mradi wa kuongeza uzalishaji wa Alizeti na Mtama waingia Singida

Posted on: May 5th, 2022

Wakulima wa zao la  mtama na alizeti mkoani Singida wapo mbioni kunufaika kupitia shughuli hizo kutokana na uanzishwaji wa Mradi wa kuongeza uzalishaji wa mazao hayo, uongezaji thamani na uhifadhi wa mazao baada ya kuvunwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Mkuu wa Mkoa huo Dkt Binilith Mahenge alipokutana na wawakilishi wa shirika la kimataifa la Chakula na Kilimo Duniani (WFP) pamoja na wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa kilimo katika ukumbi wa Mkoa huo ambapo alibainisha kwamba changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora, masoko na upotevu mazao baada ya kuvunwa vitapatiwa ufumbuzi siku chache zijazo.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge akizungumza wakati wa kikao hicho

Amesema Shirika hilo limekuja na Mradi wa kuwasaidia wakulima wa Singida kuongeza uzalishaji wa alizeti, mtama na  mazao ya bustani na vikolezo katika vijiji visivyopungua 50 na visivyozidi 70 huku akibainisha kwamba mradi huo umekuja na suluhisho la soko kwa mazao ya wakulima hao.

Aidha RC Mahenge amependekeza Mradi huo kushirikiana na Halmashauri kuzalisha mbegu za alizeti na mtama kwa kuwa Halmashauri zina uwezo na maeneo yenye kufaa uzalishaji huo.

Hata hivyo RC Mahenge akizitaja Taasisi ya Magereza kuwa mradi huo pia unaweza kushirikiana katika kuzalisha mbegu za alizeti na mtama kwakuwa wana maeneo na nguvu kazi ya kutosha ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa mbegu Bora  kwa wakulima wa Mkoa huo.

Awali akiutambulisha Mradi huo Mkuu wa Ofisi ya mahusiano Shirika la chakula duniani Neema Mina Sitta alisema Mradi una malengo ya  kuongeza uzalishaji wa mtama alizeti pamoja na mboga mboga ili kuchangamkia fursa ya soko inayopatikana katika nchi ya Sudani pamoja na viwanda vya uzalishaji wa  vinywaji hapa nchini.

Amesema Mradi utaongeza uzalishaji kwa kuboresha upatikanaji wa mbegu kutokana na ushirikiano baina yao na Shirika la utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) ambapo watazalisha mbegu mama.

Aidha Mradi huo utawaunganisha wakulima na masoko na utasaidia kuongeza thamani ya mazao ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika maeneo ya uzalishaji alisema Neema.

Kwa upande wake Afisa Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na uzalishaji Beatusi Choaji ameeleza kwamba Mkoa una wakulima wachapakazi na kazi ya uzalishaji wa mbegu unaweza kufanywa na vikundi vya wakulima ambavyo tayari vilishaundwa hivyo kuomba zoezi hilo liwe endelevu ili kuwasaidia wakulima mkoani hapo.

Hata hivyo Mhandisi Paskasi Muragili akawaomba Shirika hilo kwamba Mradi huo ujikite katika kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na kilimo cha uhakika na cha kibiashara. Huku alibainisha kwamba Wilaya ya Singida Vijijini ipo tayari kupokea mradi huo na itaendesha kikamilifu kilimo cha alizeti na Mtama.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.