• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Msikii na Munkhola watakiwa kumaliza mgogoro wa ardhi kwa majidiliano.

Posted on: February 3rd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka wananchi wa kijiji cha Msikii Kata hiyo na Munkhola Kata ya Mgori wilaya Singida vijijini kutumia njia ya majadiliano na maridhiano katika  kutatua mgogoro wa matumizi ya ardhi unaowakabili.

Dkt. Mahenge ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipofanya ziara ya kujifunza na kujionea eneo lenye mgogoro baina ya vijiji hivyo ambapo kijiji cha Munkhola wanataka eneo hilo libaki kama hifadhi ya Msitu wakati kijiji cha Msikii wakita litumike kwa ajili ya kilimo.

Aidha Dkt. Mahenge akiwa eneo hilo akawataka madiwani wa Munkhola na Msikii kukutana ili kujadili kwa kina athari zinazoweza kutokea endapo eneo hilo likitumika kwa kilimo au kwa hifadhi ya msitu ambapo watashirikiana na kamati iliyoundwa ili kupata suluhisho.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa akawasihi wananchi wa vijiji hivyo kuendelea kutunza amani utulivu na mshikamano wakati viongozi wao wakitafuta suluhisho la mgogoro huo huku akisisitiza mazao na miti iliyopandwa eneo hilo kuendelea kubaki mpaka muafaka utakapopatikana.

 “Sitapenda kusikia watu wamegombana au miti na mazao yameng’olewa wakati Serikali ipo, atakaye thubutu kuvunja amani sitakuwa na urafiki katika hilo.” Alisisitiza Dkt. Mahenge

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida vijiji  William Nyalandu akawasisitiza viongozi wa vijiji hivyo kufuata maagizo yaliyotolewa na Serikali ya kuhakikishi amani na utulivu vinakuwepo.

Hata hivyo Nyalandu akasisitizia kwamba mazao yaliyopo kutong’olewa na viongozi wahakikishe hakuna mkulima mwingine atakayeanzisha shamba jipya katika eneo hilo mpaka hapo Serikali itakapotoa muongozo.

Diwani wa Kata ya Munkhola Mhe. Dhuma Said akamuhakikishia RC Mahenge kwamba mgogoro huo utaisha kwa kutumia mijadala ya kawaida baina yao viongozi na hauwezi kwenda hatua za juu.

Hata hivyo Diwani huyo alieleza kwamba shughuli za kilimo na ufugaji zinazofanywa katika hifadhi ya msitu huo zinahatarisha maisha ya wananchi wanaozunguka eneo hilo na Mkoa kwa ujumla kwa kusababisha mmomonyoko wa udongo, jangwa na ukosefu wa mvua.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msikii Mhe. Mchaga Mtegagufa akatumia muda huo kumueleza Mkuu wa Mkoa kwamba kutokana na mgogoro huo ng’ombe Sita kutoka katika kijiji cha Msikii wamekamatwa, majembe Mawili yakukokotwa na ng’ombe hayajulikani yalipo mpaka sasa.

Hata hivyo Diwani Mchaga akamuomba Mkuu wa Mkoa waachiliwe huru watu wawili wa kijiji hicho waliokamatwa ambapo Mkuu wa Mkoa alimwagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa kuwaachia huru watu hao kwakuwa viongozi watakutana kwa ajili ya muafaka.

Ziara hiyo iliwahusisha Kamati ya Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mwenyekiti wa Halmashauri, Kamati maalum ya utatuzi wa migogoro na viongozi wa Chama cha Mapinduzi.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge mpaka wa msitu huo

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akisikiliza maoni ya wananchi katika kijiji cha Munkhola

Wanachi wa kijiji cha Munkhola na Msikii wakiwa katika eneo la msitu wenye mgogoro wa matumizi ya ardhi

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.