• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Mtandao wa Barabara waboresha maisha ya wananchi Singida

Posted on: December 2nd, 2021

Uwepo wa mitandao ya barabara kuu na za viunganishi mkoani Singida zimeongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi na kukuza uchumi wa mtu mmoja moja kutokana na biashara zinazofanyika baina ya wilaya na halmashauri mbalimbali.

Mkoa huo umetajwa kuwa na  mtandao wa barabara wenye urefu wa jumla ya  kilometa 1716.12  ambapo lami ni   Km 488.73 na changarawe ni  km  1,227.39

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge alipokuwa akifungua kikao kazi cha 44 kilichohusu Bodi ya barabara ya Mkoa  ambacho kimefanyika leo Desemba 3, 2021 katika ukumbi wa mkoa huo  na kuhusisha wakala wa barabara (TANROAD), Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wabunge wa mkoa huo, Viongozi wa CCM mkoa, wenyeviti wa Halmashauri, wakurungezi watendaji, na wataalamu mbalimbali wa Serikali.

Akiongea katika kikao hicho RC. Mahenge amesema mifumo ya barabara iliyopo katika Mkoa huo umefungua fursa mbalimbali  za kiuchumi kwa kuwa imeendelea kuunganisha Mkoa na Mikoa mingine, miji na  maeneo ya kitalii pamoja na migodi ya madini.

“Mifumo ya barabara imekuwa kama mishipa ya damu ambayo ikisimama kila kitu kina simama, nawashukuru sana TANROAD na TARURA kwa kusaidia kuboresha barabara za lami na zile zenye kiwango cha changarawe” alisema RC. Mahenge.

Aidha akawaomba viongozi waliohudhuria kikao hicho kuhakikisha wanasaidia kusimamia ujenzi wa barabara zote zinazoendelea  katika maeneo mbalimbali mkoani hapo kwa kuwa fedha nyingi za barabara zinaendelea kuja.

Aidha Mkuu wa Mkoa akaendelea kuwakumbusha wakandarasi wote wanaoshughulika ujenzi wa barabara  kuhakikisha wanatekeleza kazi zao kwa muda walipewa kwa kuwa hatapenda kusikia sababu zozote zitakazosimamisha ujenzi huo.

Akiwakilisha taaraifa yake Meneja wa TANROAD Mkoa Mhandshi Erick Ng’walali amesema hali ya barabara  katika Mkoa wa Singida  inaridhisha  kwa kuwa  asilimia 63.1 ni barabara zenye hali nzuri, asilimia 27.6 ni hali ya wastani wakati asilimia 9.3 tu zina hali  mbaya.

Aidha Mhandisi Erick akafafanua kwamba bado wameendelea kufanya matengenezo katika baadhi ya barabara mkoani hapo  ambapo asilimia 32.7 zimekamilika  na asilimia 14.4 za fedha zimekwisha tumika.

Hata hivyo Mhandisi Erick akazitaja baadhi ya changamoto zikiwemo wizi wa vyuma na alama za barabarani ambapo amesema elimu na uhamasishaji vinahitajika katika maeneo mbalimbali ili kutunza alama hizo ambazo ni muhimu kwa watumiaji wa barabara.

Aidha akatumia muda huo kuwaonya baadhi ya watu wanaotumia vibaya hifadhi ya barabara ikiwemo kupasua mifereji ya maji, kujenga na kupitisha mifugo katika sehemu ambazo hazistahili.

Akitoa maadhimio ya kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko amesema ahadi zote zilizotolewa na viongozi wa juu kuhusiana na ukarabati na utengenezwaji wa barabara utaingizwa kwenye mpango na kuhakikisha  unatekelezwa na wananchi wanafaidika.

Aidha amewataka TANROAD na TARURA kuboresha barabara na madaraja yote yenye uhitaji huo ndani ya mkoa mzima ili kuondoa athari zinazoweza kutokea wakati wa mvua.

Habari zaidi tembelea: http://singidars.blogspot.com/2021/12/mikataba-26-ya-ujenzi-wa-barabara.html

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.