• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MWENGE WA UHURU 2019 WAPOKELEWA KWA KISHINDO MKOANI SINGIDA

Posted on: August 19th, 2019

Serikali ya mkoa wa Singida inayoongozwa na mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi, kwa kushirikiana na wananchi wa Singida, mapema leo 19/08/2019 wameupokewa Mwenge wa Uhuru ukitokea mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema, Mwenge wa Uhuru 2019, Katika Mkoa wa Singida utakimbizwa kwa muda wa siku 7 katika Halmashauri 7 kwa kuanzia na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni leo tarehe 19 Agosti, 2019 na utahitimisha mbio zake mnamo tarehe 25 Agosti, 2019 na tarehe 26 Agosti, 2019 utakabidhiwa mkoani Tabora.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa, katika Mkoa wa Singida Mwenge wa Uhuru utakimbizwa jumla ya Kilometa 804.8, utapitia jumla ya miradi 46 inayohusu Sekta za Elimu, Afya, Mazingira, Maji, Utawala Bora, Kilimo, Ushirika, Biashara, na Programu za mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya, Malaria, Rushwa, Elimu ya Mpiga kura na UKIMWI.

Amesema, Miradi 12 itazinduliwa ambapo miradi 2 itafanyiwa ufunguzi, miradi 10 itawekwa jiwe la msingi na miradi 22 itakaguliwa na kutembelewa. Miradi yote itakayopitiwa itakuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania 9,462,470,874/=.

Aidha, Dkt. Nchimbi amemhakikishia mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2019 Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali, kuwa Serikali ya Mkoa wa Singida imejipanga vema katika kuhakikisha inatokomeza na kumaliza kabisa mizizi ya Rushwa, Madawa ya Kulevya, UKIMWI na Malaria kwa kutambua na kupokea Ujumbe mwambatano wa Mapambano dhidi ya Rushwa, chini ya kaulimbiu, “Kataa Rushwa Jenga Tanzania”.

Pia, Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, chini ya kaulimbiu “Shiriki kutokomeza Malaria kwa manufaa ya jamii”. Mapambano dhidi ya UKIMWI chini ya kaulimbiu “Mwananchi Jitambue, Pima afya yako sasa”.

“ Napenda kuwakaribisha rasmi Mkoani Singida vijana wetu wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2019 Kitaifa” Dkt. Nchimbi

Awali, Dkt. Nchimbi, kwa niaba ya Serikali ya Mkoa wa Singida pamoja na wananchi wote, alianza kwa kutoa salamu za pongezi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano kwa moyo wa upendo, kusimamia rasilimali za nchi, kudhibiti wizi na ubadirifu, kuongoza vema, kusimamia utekelezaji wa Agenda kubwa za Kitaifa zikiwemo; Ununuzi wa Ndege, Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere, Ujenzi wa Reli ya Mwendokasi, Elimu Bure, kutuimarisha katika undugu na Nchi za SADC, Afrika Mashariki, Afrika na Dunia.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida ametoa fedha kiasi cha Shilingi za Kitanzania Laki moja na shilingi 40 elfu kwa ajili ya kuboresha vyoo vya shule ya msingi Sanza. Fedha hizo zilipatikana wakati mkuu huyo wa Mkoa akiimba wimbo wa kuiburudisha jamii na kuielimisha juu ya Mwenge wa Uhuru 2019, wimbo uliopelekea jamii kuguswa na kuweza kumtunza Mkuu huyo wa Mkoa.


Imetolewa Na;

Kitengo cha Habari na Mawasiliano 

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

SINGIDA

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.