• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

NAIBU WAZIRI JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUPELEKA VIJIJINI, TEKNOLOJIA NA PEMBEJEO BORA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI.

Posted on: August 9th, 2017

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Suleiman Jafo amezitaka halmashauri zote nchini kutekeleza jukumu lao la kuwapelekea wakulima wa vijijini teknolojia na pembejeo bora ili kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji mali.

Jafo ametoa rai hiyo jana wakati wa kilele cha maonyesho ya nanenane kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma ambapo alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali yalioonyesha shughuli za kilimo na ufugaji pamoja na sekta binafsi zinazosaidia katika kukuza uchumi.

Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu ni “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” hivyo basi halmashauri zinatakiwa kuhakikisha mazao ya wakulima na wafugaji yanapata soko kwa kutoa elimu ya kuchakata na kufungasha bidhaa zao katika ubora unaokubalika sokoni ili mazao hayo yawe na thamani zaidi.

Jafo amesema halmashauri zote zinapaswa kutekeleza wajibu wao kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa na huduma zote za msingi kama vile miundombinu ya Barabara, Umeme na Maji ili kuwavutia wawekezaji na hivyo kumsaidia mkulima na mfugaji kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Ole Nasha ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa kuendelea kuwezesha shughuli za kilimo nchini huku akitoa angalizo la kutowasahau wakulima wasio na uwezo.

Ole Nasha amesema Benki hiyo isitoe mikopo kwa wakulima wakubwa na wenye uwezo tu bali isisahau jukumu la kuwafikia wakulima wasio na uwezo ili waweze kupata mikopo na kuweza kulima kisasa kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Wakati huo huo Naibu waziri Jafo ametoa Wito kwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuamua kuufanya Mkoa wa Dodoma hasa Viwanja vya Nzuguni kuwa Kituo cha Kudumu cha Maonesho ya nanenane kitaifa kutokana na Kijiografia kuwa katikati na Makao Makuu ya nchi na hivyo kuwa rahisi kwa Kanda zote nchini na hata nchi za jirani kuja kushiriki Maonesho ya Nane Nane.

Jafo amesema hayo akiunga mkono kauli iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba aliyesema Serikali inafikiria kuachana na utaratibu wa kuhamisha  hamisha Maonesho ya kitaifa ya Nane Nane kwenye Kanda mbalimbali na badala yake kuwa na kituo kimoja cha Kitaifa kama ilivyo kwa maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanavyofanyika Dar es Salaam pekee.

Jafo amesema Uwanja wa Nane Nane Nzuguni unahitaji kufanyiwa uwekezaji na uendelezaji wa miundombinu yake kama barabara, umeme na maji na kuboreshwa huduma mbalimbali na kuzitaka Mamlaka za Serikali za Mikoa ya Dodoma na Singida kuweka mkakati wa kuendeleza miundombinu hiyo kwa kuwa baada ya uwekezaji mkubwa uwanja huo utarejesha mapato mengi.

Ameongeza kuwa Serikali za Mikoa ya Singida na Dodoma inaweza kufanikisha ukarabati huo kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi kama Benki ya Uwekezaji TIB na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.

Washindi wa Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yaliyoanza tangu Agosti Mosi ni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililoibuka kuwa Mshindi wa jumla wa Maonesho ya Mwaka huu, likifuatiwa na Benki Kuu ya Tanzania ikiwa mshindi wa pili na Mshindi wa tatu akiwa ni Jeshi la Magereza.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.