• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

NAIBU WAZIRI MKUU APONGEZA PAREDI YA MIFUGO KWENYE MAONESHO YA KIMATAIFA YA NANE NANE JIJINI DODOMA.

Posted on: August 5th, 2024

Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko, amewaagiza Maafisa ugani kote nchini kuhakikisha wanatoa elimu bora na stahiki kwa Wafugaji, Wakulima na Wavuvi kama hatua ya kuongeza tija ya uzalishaji katika sekta hizo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya masoko ya ndani na la Kimataifa.

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa kauli hiyo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, (5 Agosti, 2024 ) katika ufunguzi wa mashindano ya paredi ya mifugo mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa paredi ya mifugo huchangia kuhamasisha, kukuza na kuendeleza ufugaji bora katika kuchangia katika maendeleo ya Taifa na mtu mmoja mmoja.

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko, katika ufunguzi wa mashindano ya paredi ya mifugo mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

“Mifugo ni utajiri fugeni kisasa mtaona matunda yake haraka,” Amesisitiza Biteko 

Amesema ufugaji wenye tija kwa kutumia teknolojia na mbinu za kisasa utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi hasa wafugaji, wakulima na wavuvi kuongeza vipato maradufu na kuchangia pato la taifa kwa kiwango kikubwa.

Biteko ameeleza kuwa mafanikio hayo yatafikiwa iwapo tu Maafisa Ugani kote nchini watawajibika ipasavyo katika utoaji wa elimu ya ufugaji wa kibiashara utakaosaidia kukidhi mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wao, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde, wamewahakikishia wananchi kuwa Serikali inaendelea kuweka mipango na mikakati madhubuti ili kuhakikisha sekta hizo zinaongeza tija katika uzalishaji kama hatua ya kuwaondoa wananchi na umaskini wa kipato.

Mashindano ya Paredi ya Mifugo yamekuwa kivutia kikubwa kwa wananchi kwa sababu hujumuisha mifugo bora yenye umri mdogo kati ya miaka Mitatu hadi Minne ambayo imefugwa kisasa kwa kuwa na kilo kati ya 700 hadi 800 pamoja na ng’ombe wanaotoa maziwa mengi.

Kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na zaidi ya ng’ombe Milioni 37, Mbuzi Milioni 27.6, Kondoo Milioni 9.4 na Kuku Milioni 103.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.