• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

ONGEZEKO LA TALAKA NA WATOTO WA MITAANI KUTAFUTIWA MWAROBAINI WAKE SINGIDA

Posted on: January 22nd, 2025

Viongozi wa BAKWATA Mkoani Singida wameazimia kutoa elimu kuhusu maisha ya ndoa kwa wakazi wa Singida lengo likiwa ni kupungua mmomonyoko wa maadili katika jamii pamoja na kuondoa ongezeko la Talaka na Watoto wa mitaani.

Hayo yamezungumzwa leo na Viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Singida walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego na kuzungumza kuhusu azma yao ya kutoa elimu hiyo kwa wananchi.

Akizungumzia suala hilo,Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, amesema ni wakati sahihi kuhakikisha elimu inatolewa kwa jamii ili kuondoa tabia mpya zisizofaa na kuonekana za kawaida katika jamii yetu kwa kuzikomesha ili kukwepa madhara yake mengi ikiwemo kutalikiana kwa wazazi jambo linalopunguza upendo na amani kwa watoto wao huku wengi wakikosa mahitaji muhimu kama elimu na uangalizi wa karibu yaani malezi bora.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Dendego ameahidi kutoa ushirikianao wa kutosha kwa viongozi hao wa dini kwa kuhakikisha elimu inatolewa na inawafikia wanajamii wote huku akiimba viongozi na wazazi kushirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha vijana wanarudi katika mienendo bora na kuishi katika imani kwa lengo la kuwa mfano wa kuigwa sio kwa wenzao pekee bali jamii na Taifa kwa ujumla.

Pia amewaasa wanajamii kuepuka kutengeneza makundi ya chuki baina ya wazazi kwasababu ya talaka kwani huleta madhara mengi mabaya kwa wote wanaowazunguka hususani watoto ambao bila malezi bora huishia katika mienendo isiyofaa.

"Familia ndio jamii, Ukishakuwa na familia bora utazalisha jamii bora"Amesema Mhe.Dendego.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekua na ongezeko la ndoa nyingi kuvunjika kwa sababu mbalimbali huku ikidaiwa kuchochewa na mporomoko mkubwa  wa maadili inayochangiwa na malezi yasiyofaa na matumizi mabaya ya Teknolojia.Kwa kutoa elimu ya maadili katika jamii pamoja na maadili katika ndoa kutapunguza pasi na kuondoa kabisa utoaji wa talaka ambao utakuwa moja ya sababu kubwa ya kukuza maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla kutokana na utulivu utakaokuwepo utakaotoa muda mrefu wa uzalishaji mali.


@USIKOSE KUFUATILIA MITANDAO YETU YA KIJAMII

INSTAGRAM:SINGIDA RS

FACEBOOK:SINGIDA RS

YOUTUBE:RAS SINGIDA 

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • ANUANI ZA MAKAZI KUJA NA FURSA LUKUKI ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

    May 26, 2025
  • WANAFUNZI NI SALAMA CHINI YA MRADI WA SHULE BORA .

    May 26, 2025
  • WAAJIRI WATAKIWA KUVIONGEZEA NGUVU VITENGO VYA MAWASILIANO SERIKALINI

    May 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.