Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ameendelea na Ziara ya ukaguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida leo Mei 15,2025 akikagua miradi iliyokamilika na ile inayoendelea maeneo mbalimbali.
Ukaguzi ulianzia katika Mradi wa Maji Katika Kijiji cha Nsunsu,Kata ya Ntwike,Tarafa ya Shelui mradi ulioanza kutekelezwa Mei 2024 na kukamilika Novemba 2024 kwa kutumia wataalamu wa RUWASA.Mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi 415,993,640 na una ujazo wa lita 50,000.
Kikundi cha Vijana 'NGUVU MOJA'kilichopo kilichopo Kata ya Tyegelo Kata ya Kidaru kilichopata mkopo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kiasi cha Shilingi 7,000,000 uliowezesha kikundi hicho kununua eneo la shamba ekari 4 kwa ajili ya mashine,kulipia eneo la kulima mpunga ekari 4 na kiasi kingine kuendeshea biashara ya kununua na kuuza mpunga.
Kikundi hicho baada ya kumaliza marejeaho ya mkopo wa awali kimeomba mkopo wa awamu ya pili wa Shilingi 22,000,000 ili kuweza kununua mashine ya kukoboa mpunga,kujenga jengo la kusimika mashine,kununua mpunga na kuuza mchele.
Ujenzi wa chumba kimoja cha Darasa Shule ya Msingi Luono iliyopo katika Kata ya Kidaru,Tarafa ya Kisiriri inayojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri itakayogharimu kiasi cha Shilingi 23,000,000 ambapo utahusisha ujenzi wa Chumba kimoja cha darasa,utengenezaji wa madawati 15,meza moja na kiti cha Mwalimu ambapo wanafunzi 45 watatumia darasa hilo.
Ujenzi wa Shule mpya ya Awali na Msingi Yombo iliyopo katika Kijiji cha Tulya,Tarafa ya Kisiriri.
Umehusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 7 vya Msingi,madarasa mawili ya Elimu ya Awali,matundu ya vyoo,kichomea taka,Jengo la utawala,Uzio wa Madarasa ya Awali na Viwanja vya Michezo.
Mradi huu unatarajiwa kuhudumia wanafunzi 272 wa madarasa ya awali na 226 wa Shule ya Msingi na kuwaepusha kutembea umbali mrefu kupata elimu hasa wanaotoka Vitongoji vya Yombo na Bambalaga.
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Konkilangi kwa Mita 50,barabara ya maingilio yenye kilometa 1.5 kwa kiwango cha changarawe katika barabara ya Mkoa ya Shelui-Sekenke-Tulya-Tyegelo.Mradi huu upo katika Kijiji cha Konkilangi,Kata ya Ntwike unaogharimu kiasi cha Shilingi 6,698,257,300 ambapo unatarajiwa kuunganisha Mkoa wa Singida na Ukanda wa Ziwa kupitia daraja la Mto Sibiti ambalo limekwishakukamilika.
Ujenzi wa Zahanati mpya ya Mseko katika Kata ya Mgongo Tarafa ya Shelui ukihusisha ujenzi wa jengo la OPD&RCH,ujenzi wa jengo la wazazi,nyumba ya watumishi,ujenzi wa choo,kichomea taka,shimo la majivu,uzio pamoja na ujenzi wa mnara wa maji.Mradi huu unagharimu kiasi cha Shilingi 250,000,000 na unatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 3,337.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.