• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RAS Mwaluko azindua wiki ya utumishi wa umma ki Mkoa, ahimiza viongozi kutimiza wajibu wao na kutoa huduma stahiki kwa mujibu wa sheria katika kuwahudumia Wananchi.

Posted on: June 17th, 2022

VIONGOZI wa Taasisi za Umma na binafsi mkoani Singida, wamehimizwa kuhakikisha wanajenga mazingira rafiki baina yao na watumishi wanaowaongoza ili kuongeza tija na uwezo wa kutoa huduma mbalimbali zitakazo kidhi mahitaji ya wananchi.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Singida uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa mkoa huo Juni 16, 2022.

Amefafanua kwamba wiki ya Utumishi wa umma inalenga kuhamasisha na kuwakumbusha watumishi wa sekta ya umma na binafsi kujua wajibu wao katika kuwahudumia wananchi pamoja na kutambua miiko mila na desturia za utumishi wa umma ambazo zitasaidia kuongoza mahusiano mazuri katika kutekeleza majukumu ya kazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza na Viongozi wa Taasisi za Umma na Binafsi pamoja na Vyama vya Wafanyakazi mkoa wa Singida katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo tarehe 16 Juni, 2022

“Ili wananchi waweze kuhudumiwa ipasavyo kiongozi wa Taasisi ni lazima awe na mahusiano mazuri na watumishi anaowaongoza. Pia awe na utamaduni wa kuwatembelea watumishi wa chini yake na kujua changamoto zinazowakabili. Changamoto ambazo zipo kwenye uwezo wao wazitatue mapema iwezekanavyo”. Amesisitiza Mwaluko.

Amewasisitiza kutoa huduma kwa wananchi bila upendeleo au ubaguzi wowote na pale wanapokutana na changamoto ambazo zitakuwa juu ya uwezo wao waziwakilishe kwenye mamlaka husika ili ziweze kutafutiwa majibu.

“Wapo baadhi ya viongozi wa taasisi za umma au binafsi hawapo karibu na watumishi wa chini yao. Mtumishi akifanya kakosa kadogo kiongozi badala ya kusaidia kutatua anatishwa na kuambiwa atachukulia hatua kali dhidi ya mtumishi huyo. Tabia hii haijengi na haivumiliki kabisa”. amesema RAS Mwaluko.

Mwaluko amesema ni kweli tunapashwa kusimamia sheria kanuni na taratibu lakini wakati mwingine busara zinatakiwa zitumike hasa ukizingatia  binadamu ni mtu wa makosa.

Aidha, ameonya viongozi wengi wa taasisi za umma na binafsi ambao hawajishughulishi na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi walio chini yao kitendo hicho kinachochea watumishi hao kukimbilia ofisi ya Katibu Tawala Mkoa ambayo imegeuka kuwa kama kliniki.

“Tarehe 23 mwezi wa Nane Sensa tujiandae kuhesabiwa na tukawahimize wananchi wanaokuja kupata huduma kwetu ili waweze kutambua hiyo tarehe kwa ajili ya SENSA ya mwaka huu”. Amesisitiza Dorothy Mwaluko

Kwa upande wake Katibu Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Mwalimu Suzan Shesha ametumia nafasi hiyo kumshukru na kumpongeza Katibu Tawala Mkoa huo Dorothy Mwaluko kwa kubuni na kuanzisha wiki ya utumishi wa umma ambayo itasaidia katika kubadilishana uzoefu na kuongeza hali ya utendaji katika kuwahudumia wananchi.

“Kukutanisha viongozi wa taasisi za umma na binafsi mama yetu Dorothy Mwaluko ameona mbali sana. Sisi viongozi tumepata nafasi ya kutoa changamoto zinazotukabili na zimepatiwa majibu wakati huo huo. Ili kumuunga mkono Katibu Tawala wetu tunaenda kuhakikisha walimu wanawajibika ipasavyo”. Amesema Suzan Shesha

Aidha, Suzan ametumia fursa hiyo kumshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mambo mengi mazuri anayowatendea watumishi wakiwemo walimu katika kutatua changamoto mbalimbali pamoja na ile sugu ya kupandishwa madaraja.

Naye, Katibu Chama cha walimu Wilaya ya Mkalama, Amani Msange amesema yale yote aliyoagiza Katibu Tawala Mkoa wanaenda kuyafanyia kazi ikiwemo kutembelea watumishi  na kujua changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza na Viongozi wa Taasisi za Umma na Binafsi pamoja na Vyama vya Wafanyakazi mkoa wa Singida katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo tarehe 16 Juni, 2022

Katibu Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Mwalimu Suzan Shesha akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano mara baada ya Uzinduzi wa wiki ya Utumishi wa Umma uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo tarehe 16 Juni, 2022

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.