• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RAS SINGIDA AAGIZA WAATHIRIKA WALIOACHA KUTUMIA DAWA ZA KUFUBAZA VIRUSI VYA UKIMWI WATAFUTWE

Posted on: April 18th, 2024

Serikali Mkoani Singida imeagiza Waganga Wakuu wa Wilaya na Wadau wengine wa Afya kuwatafuta na kuwarejesha katika matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI kwa waathirika 857 ambao wameacha kutumia dawa hizo katika Halmashauri Tatu (3) za Itigi, Ikungi na Singida.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga wakati anafungua kikao cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi wa USAID AFYA YANGU ambao unatekelezwa Mkoani humo.

Katibu Tawala huyo wa Mkoa ameonyesha kutoridhishwa na idadi hiyo kubwa ya watu wanaotuma dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI kuacha kutumia dawa hizo na amesisitiza kuwekwa kwa mikakati na mipango madhubuti itakayosaidia kurejesha kundi hilo katika matumizi ya dawa hizo haraka iwezekanavyo.

Amesema kuna umuhimu wa kutengeneza mahusiano mazuri kati na watoa huduma na wateja wao ikiwemo kuwapigia simu pindi wanapoona mteja wao hafiki kuchukua dawa ili kujua sababu ambazo zinamfanya asiende kuchukua dawa hizo ili kuona namna bora ya kumsaidia.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovick, ametaja sababu zinazopelekea idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI mkoani humo kuacha kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo kuwa ni waathirika hao kuhama na kwenda maeneo mengine na umbali kutoka kwenye makazi yao hadi kwenye vituo vya kutolea huduma hizo.

Ludovick amesema mpango uliopo kwa sasa ni kuhakikisha watumiaji hao wa dawa za kufubaza virusi hivyo wanatafutwa popote walipo na kuwapa ushauri nasaha kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa hizo kwa ajili ya afya zao.

Naye, Meneja Mradi wa USAID AFYA YANGU mkoani Singida, Said Mgeleka, amesema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika Mkoa huo ambapo umeweza kusaidia kuibua watu zaidi ya 700 walioathirika na virusi vya UKIMWI kila baada ya miezi Mitatu na kuwaazishia dawa haraka mara baada ya kugundulika.

Mradi wa USAID AFYA YANGU unatekelezwa katika Mikoa Sita (6) ya Tanzania Bara ambayo ni SINGIDA, DODOMA, MANYARA, TABORA, ARUSHA na KILIMANJARO.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.