• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RAS SINGIDA, DKT. ANGELINA LUTAMBI, AMEZINDUA KAMPENI YA MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI NA KUWATAKA WANANCHI KUWA NA UTARATIBU WA KUPIMA AFYA.

Posted on: May 29th, 2019

Serikali mkoani Singida, imewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini magonjwa ambayo yanachukua muda mrefu kujitokeza, na kuacha tabia ya mtu kusubili hadi afya iwe na mgogoro ndipo akapime.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mapambano dhidi ya Saratani mkoani Singida.
Dkt. Lutambi amesema, ugonjwa wa Saratani ukibainika katika hatua zake za awali, upo uwezekano wa kutibika endapo mgonjwa atazingatia kikamilifu ushauri wa wataalamu.
“Ni vema kila mmoja wetu kuwa na desturi ya kupima afya mara kwa mara ili kutambua hali ya kiafya. Endapo utatambulika una ugonjwa wa Saratani, hakikisha unapata huduma za afya kulingana na ushauri utakaopewa  na wataalamu wa Afya”.
Amesema, wale waliokwisha jitambua kuwa na saratani, waendelee kutumia  huduma za afya ili kuepuka athari zitokanazo na ugonjwa huo hatari wa saratani.

Akitaja baadhi ya vyanzo vya ugonjwa wa saratani, Dkt. Lutambi amesema, vyanzo vikubwa vya saratani ni pamoja na matumizi ya tumbaku na bidhaa za ugoro.

“Matumizi ya tumbaku ni kisababishi kikubwa cha magonjwa ya Saratani ya Matiti, mdomo, koo pamoja na ugonjwa wa moyo. Pia unywaji wa pombe  uliopitiliza kusababisha magonjwa ya Saratani ya Matiti, Ini, Utumbo mpana, pamoja na saratani nyingine.
Aidha, amewataka wananchi kujiepusha na visababishi vya ugonjwa huo wa Saratani kwa kuwa ni ugonjwa hatari kwa maisha ya binadamu.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Singida, kwaniaba ya wananchi wa mkoa wa Singida, ameishukuru taasisi ya Saratani ya hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es salaam kwa kutuma madaktari kuja kutoa huduma za kitabibu kwa wakazi wa mkoa wa Singida.
Awali, Meneja kitengo cha uchunguzi wa Saratani hospitali ya Ocean Road, Dk. Maguha Stephano, amesema pamoja na kutoa huduma ya afya, pia wametoa mafunzo ya awali  juu ya kutambua saratani kwa baadhi ya wataalamu wa afya mkoa wa Singida, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutambua saratani.


“Taasisi yetu ya Ocean Road inatembea kwa maono ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya TANO, Dkt John Magufuli na ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo ni Watanzania kuwa na afya njema”. Dk. Maguha Stephano.
Wakati huo huo mkazi wa Mtaa wa Munugh’una Manispaa ya Singida, Bi. Mwanaidi Kipandwa, ameishukuru taasisi ya Ocean Road, kwa uamuzi wake wa kusogeza karibu huduma ya utabibu kwa kuitoa bure kwa wakazi wa mkoa wa Singida.
“Wengi wetu hapa tulipo  kufika Dar es salaam ni mtihani mkubwa. Naiomba taasisi ya Ocean Road isichoke, ijenge utaratibu wa kuleta au kusongeza  huduma hii muhimu sana kwetu sisi tusio na  uwezo wa kufuata huduma za matibabu Dar es salaam”, Amesema Bi. Mwanaidi Kipandwa.


Kampeni hii inatekelezwa kwa siku tano mkoani Singida na timu ya wataalamu kutoka hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es salaam.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.