• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC DENDEGO ASISITIZA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA WADAU WA KILIMO.

Posted on: February 6th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na wadau wa maendeleo kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya kilimo ili kuhakikisha matokeo chanya na endelevu kwa wananchi. 

Ameyasema hayo Februari 6, 2026 wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utendaji wa wadau wa mradi unaotekelezwa na Shirika la HELVETAS, kilichofanyika katika Ukumbi wa Amenity Hotel, Manispaa ya Singida.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Dendego ameeleza kuwa taarifa na takwimu zinazowasilishwa na wadau wa maendeleo ni nyenzo muhimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya Serikali, hivyo zinapaswa kuchambuliwa na kuingizwa kikamilifu katika mipango ya Halmashauri na Mkoa. Amesema hatua hiyo itawezesha kufanya tathmini ya kina ya mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo na mwelekeo wa maendeleo, sambamba na kuboresha utoaji wa huduma kwa wakulima na wadau wa sekta ya kilimo.

Aidha,  amesisitiza kuwa Serikali ina wajibu wa kuhakikisha miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na wadau kama HELVETAS inasimamiwa ipasavyo na kurasimishwa katika mifumo ya Serikali ili matokeo yake yaendelee kuwafaidisha wananchi hata baada ya kukamilika kwa miradi husika. Ameeleza kuwa jitihada hizo zina mchango mkubwa katika kuimarisha kilimo endelevu, kuongeza uzalishaji, kulinda mazingira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi mkoani Singida.

Vilevile,  amewahimiza wakulima, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kutumia ipasavyo elimu na teknolojia wanazopewa kupitia miradi ya maendeleo, akisisitiza umuhimu wa ubunifu, uchapakazi na uwajibikaji akisema kwa kufanya hivyo, Mkoa wa Singida utaendelea kupiga hatua katika uzalishaji wa kilimo, uanzishaji wa viwanda vidogo na kuongeza fursa za ajira kwa wanawake, vijana na makundi yenye mahitaji maalum, hatua itakayochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Mkoa.

Kwa upande wake, Afisa kutoka Shirika la HELVETAS mkoani Singida amesema shirika hilo linaendelea kutekeleza miradi inayolingana moja kwa moja na vipaumbele vya Mkoa wa Singida, hususan katika maeneo ya kilimo endelevu na uchumi wa kijani, uwezeshaji na uhifadhi wa rasilimali za asili pamoja na uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi. 

“HELVETAS inalenga pia kuimarisha ushiriki wa wananchi katika mipango na maamuzi ya maendeleo ili kujenga jamii zinazojitegemea, zenye ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na zinazoshiriki kikamilifu katika maendeleo endelevu ya Mkoa wa Singida.” Amefafanua.

Na kwa upande wa wadau waliohudhuria kikao hicho, wamesema mradi wa HELVETAS umewajengea uwezo mkubwa katika uzalishaji na uongezaji thamani wa mazao. Wameeleza kuwa kupitia mafunzo waliyopata wamejifunza mbinu bora za kilimo, utengenezaji wa mbolea na usindikaji wa mazao, hali iliyowawezesha kuongeza tija shambani na kuboresha ubora wa bidhaa zao.

“Kupitia mradi wa HELVETAS tumepata elimu nyingi ikiwemo mbinu bora za kilimo na usindikaji. Kwa sasa tuna kiwanda kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kinachotusaidia kusindika bidhaa zetu, na tukipata ithibati ya TBS tutaweza kupanua masoko yetu ndani na nje ya Mkoa.” wamesema.

Kikao hicho ni jukwaa muhimu la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo, likiwa na lengo la kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo, kuongeza kipato cha wananchi na kuifanya Singida kuwa mkoa wa mfano katika utekelezaji wa kilimo endelevu na uchumi wa kijani.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC DENDEGO ASISITIZA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA WADAU WA KILIMO.

    February 06, 2026
  • MAAFISA UGANI WAASWA KUWA WATATUZI KERO ZA WAKULIMA SHAMBANI

    February 02, 2026
  • TSH. 27,000/- PEKEE KUWASHA UMEME KILA KAYA.

    February 03, 2026
  • SINGIDA YAWEKA MKAZO KILIMO CHA ALIZETI NA MALEZI BORA KWA WATOTO

    February 01, 2026
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.