• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Mahenge Akagua Usambazaji wa Mbegu za Alizeti Kwa Wakulima

Posted on: January 11th, 2022

Wakulima Kata ya Muhalala Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wametakiwa  kuongeza kasi ya ununuaji wa mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi zikiwemo  alizeti, mtama na viazi wakati wakisubiri mvua ambazo zinatarajiwa kunyesha chini ya kiwango ili kuhakikisha wanapata mazao ya biashara na chakula.

Akiongea wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo 11 Januari 2022 katika Kata hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ametoa kauli hiyo wakati akikagua hali ya usambazaji wa mbegu za alizeti zenye ruzuku ya Serikali kwa wakulima wa Manyoni ambapo imeonekana Kata hiyo wakulima wamenunua kilo 245  tu kati ya kilo 2650 zilizopangwa katika Kata hiyo.

Aidha Dkt. Mahenge akawataka Maafisa Kilimo kuongeza uhamasishaji na elimu juu ya matumizi ya mbegu bora na umuhimu wa kilimo cha alizeti kwa mkoa huo ambapo wanatakiwa kununua mbegu hizo kwa gharama ya Sh. 3500 kwa kilo.

“Serikali imeweka ruzuku kwenye mbegu za alizeti badala ya kuuzwa shilingi 15000 watanunua kwa sh. 3500 hivyo kila mkulima anunue mbegu wakati akisubiri  mvua”.  Alisema RC Mahenge

RC Mahenge akafafanua kwamba wataalamu wa hali ya hewa wamebainisha kwamba kiwango cha mvua kitakachopatikana kwa mkoa wa Singida ni cha wastani ambacho kitafaa baadhi yakiwemo alizeti na mtama.

Dkt. Mahenge  akawakumbusha wananchi wote wa Mkoa huo kupitia mkutano wake na wananchi wa Muhalala  kutunza na kutumia chakula vizuri kwa kuwa hali ya hewa inaonesha kwamba  msimu ujao  kutakuwa na upungufu wa mazao ya  chakula kutokana na upungufu wa mvua msimu huu.

“Endapo tukilima alizeti, mtama na viazi mazao haya kwa kuwa yanachukua muda mfupi kukomaa na yanahitaji mvua kidogo, yatatusaidia kupata chakula na fedha, kwa kufanya hivyo mkoa wa Singida hatutakuwa kwenye hatari ya upungufu wa chakula”. Alikaririwa RC Mahenge.

Naye Katibu Tawala Msaidizi  sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani hapa Bw. Beatus Choaji amesema Wilaya ya Manyoni imepata jumla ya tani 48 za mbegu za alizeti ambapo tani 40 tayari zimesambazwa katika Kata mbalimbali.

Aidha amebainisha kwamba mbegu hizo zinatolewa kwa mkopo kwa wakulima ambapo watakuja kulipa baada ya mavuno japo wenye uwezo wa kununua watapatiwa  huduma hiyo alisisitiza Bwana Choaji.


Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala amesema bado wanaendelea kuhamasisha wakulima katika kata mbalimbali wilayani hapo ili kununua mbegu za alizeti japo bado wakulima wengi walikuwa hawajajitokeza kwa sababua walihofia mvua ya msimu huu kuwa kidogo.

Bwana Chimsala akaendelea kusema kwamba Wilaya kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Kilimo wameendelea kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya namna bora ya kutunza na kuhifadhi chakula ili kuwasaidia wakati wa mahitaji.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa akizungumza wakati wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.