MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Iramba mkoani hapa ikihusisha ujenzi wa vituo vya afya, shule na visima vya maji lengo likiwa ni kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi na kuondoa msongamano.
Akiongea leo na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Iramba Rc Mahenge ametaja miradi inayotekelezwa kwamba ni ujenzi wa shule ya Sekondari Maluga inayotarajiwa kugharimu kiasi cha Tsh. Milioni 470, ujenzi wa vituo vya Afya vinne (4) vya Tyegelo, Kisiriri, Mwanduigembe na Ndulungu pamoja na ujezi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari za Tulya na Kisiriri ambavyo kwa ujumla wake vinagharimu kiasi cha Tsh. Bilion 1.525 zitokanazo na tozo ya miamala ya simu.
Aidha RC Mahenge akawataka wasimamizi na wahandisi wa miradi mbalimbali wilayani hapo kuiga mifano ya miradi inaotekelezwa na Wakala wa usambazaji wa maji Vijijini na usafi wa mazingira (RUWASA) ambapo wamekuwa wakisimamia miradi yao kwa ufanisi na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.
Katika taarifa yao RUWASA imeonesha kwamba katika Wilaya ya Iramba wana miradi mikubwa mitano (5) katika vijiji vitano vya Maluga, Zinziligi, Kisiriri, wembere na Kaselya pamoja na uchimbaji wa visima 24 katika vijiji mbalimbali ambapo miradi yote inagharimu kiasi cha Tsh.Bilion 3.304 na imetekelezwa kwa asilimia 70.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huyo, DC wa Iramba Suleimani Mwenda alisema Wilaya imepokea jumla ya Tsh.Bilion 1.119 kwa ajili ya Ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vinne huku ikipokea jumla ya Tsh. Milioni 940 kwa ajili ya Ujenzi wa shule mpya za Kata ya Maluga na Ndulungu.
Hata hivyo DC Mwenda akabainisha kwamba Wilaya ya Iramba imepata fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 1.473 zitokanazo na ruzuku kutoka Serikali kuu ambapo zinatumika katika Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mtoa na ukamishaji wa madarasa 10 ya shule za msingi.
Aidha fedha hizo zinatumika pia katika Ujenzi wa madarasa Sita katika Shule za Sekondari sita pamoja na ukamilishaji wa vyumba 10 vya Maabara katika Shule za Sekondari tano wilayani hapo aliendelea kusema DC Mwenda.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati alipotembelea kujionea ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri wilayani Iramba
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.