• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC MAHENGE ARIDHISHWA UKUSANYAJI, UDHIBITI MAPATO SINGIDA DC

Posted on: October 20th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ameridhishwa na hatua kadhaa zinazoendelea kuchukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika nyanja za udhibiti, kasi ya ukusanyaji na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato ambavyo vimewezesha kupaisha mapato kutoka 60.9 milioni mwezi Julai mwaka huu hadi kufikia milioni 139.3 mwezi Agosti.

Aidha, Dk. Mahenge amepongeza uamuzi wa halmashauri hiyo kutoa eneo la ekari 50 kwa Amcos ya wazalishaji zao la Mkonge iliyopo Kata ya Mudida Kijiji cha Mpipiti, ambapo pamoja na mambo mengine, ameahidi kuhakikisha anawaunganisha kikamilifu na Bodi ya Mkonge nchini ili kuwawezesha kuanza kunufaika na bei ya soko.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanaainisha vyanzo vyote vya mapato na kuvifanyia tathmini ili kubaini kila chanzo kihaulisia kinapaswa kukusanya kiasi gani gani cha fedha, kuweka usimamizi na udhibiti madhabuti, lengo ni kuwezesha vyanzo husika kuanza kukusanya mapato kwa asilimia 100.

“Nimeridhika na taarifa yenu hasa ya mapato, kikubwa hapa kaeni tengenezeni timu fanyeni analysis ya uhalisia wa kila kinachofanyika na kukusanywa kwenye vyanzo vyote rasmi na visivyo rasmi…tuwe na shabaha kwa kila tunachokifanya,” alisema

Kuhusu uzalishaji wa zao la mkonge ambalo baada ya kuoteshwa limeonesha kutoa matokeo chanya na ubora wa hali ya juu kwenye ardhi ya Mkoa wa Singida, hususani ndani ya halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa aliwahamasisha wana-singida na watakaohitaji kuwekeza kuchangamkia fursa ya zao hilo ambalo uwekezaji wake hauhitaji nguvu kubwa lakini faida yake ni kubwa.

“Uzuri wa mkonge hauna changamoto yoyote ukishapanda basi wewe unasubiri kuvuna tu…hivyo unaweza kulima mkonge na wakati huohuo ukaendelea na kilimo chako cha mazao mengine. Na mkonge wetu wa singida umeonekana kuwa bora zaidi na kimbilio kuliko maeneo mengine nchini,” alisema

Katika hilo, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri alimweleza Mkuu wa Mkoa kwamba kwa sasa wakulima wa wilaya hiyo wanaozalisha mkonge wanapata tabu kubwa kutokana kulazimika kuuza kwa madalali ambao huwalangua, hivyo alipendekeza waanze kuuza kwa bodi ili kupata bei ya soko sambamba na halmashauri kupata mapato halisi na hatimaye wawekezaji wengi waweze kuja.

Pia katika hatua nyingine kupitia ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Elia Digha alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa namna alivyoonesha kuipenda na kuijali halmashauri kwa kuipatia shilingi bilioni cha 1.6 kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya elimu, afya na maji sanjari na fedha nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa kwa kipindi tofauti kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Awali akizungumzia fedha hizo, pamoja na kumpongeza Rais Samia, Dk. Mahenge aliwaasa watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanazitumia fedha hizo kwa malengo kusudiwa.

“Niwasihi sana fedha hizo ni za moto…hazina posho wala urafiki. Hakikisheni kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa na kwa viwango na ubora stahiki,” alisema Mahenge

Dkt. Mahenge (kulia) akipokea maelezo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida unaoendelea. 

Dkt. Mahenge akitazama nyuzi za mkonge zenye ubora wa hali ya juu muda mfupi baada ya kuzalishwa katika kijiji cha Mpipiti Kata ya Mudida.

Baadhi ya watendaji na viongozi wa chama na Serikali wakimsikiliza Mkuu wa mkoa Dkt. Mahenge (hayupo pichani) wakati wa kikao cha ndani alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri, akizungumza katika moja ya Shamba la Wakulima wa zao la Mkonge AMCOS ya kijiji cha Mpipiti Kata ya Mudida wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akitoa maelekezo ya namna ya kuongeza tija na uzalishaji wa zao la Mkonge katika Kijiji cha Mpipiti Kata ya Mudida wilayani Singida vijijini alipofanya ziara yake ya kikazi Oktoba 21, 2021. Zao hilo limeonesha matokeo chanya kwa ardhi ya mkoa wa Singida, hususan ndani ya Halmashauri ya Singida vijijini.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.