• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Mahenge atembele ujenzi wa Barabara ya Rungwa, Itigi na Mkiwa, awataka wananchi kutunza Mazingira.

Posted on: November 10th, 2021

Wananchi wa Halmashauri ya Itigi katika Kata ya Rungwa wametakiwa kutunza Mazingira kwa kupanda miti ambayo itasaidia kupunguza uharibifu wa Mazingira na kulinda  barabara  ambayo inaendelea kutengenezwa.

Kulingana na Mazingira ya Rungwa Barabara zimekuwa zikiharibika kutokana na kukatwa  miti  na kusababisha mmomonyoko wa ardhi na maji kuhama katika mikondo yake.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ameyasema hayo tarehe 9.11.2021 alipofanya ziara ya kukagua barabara ya Rungwa, Itigi na Mkiwa yenye urefu wa Kilomita zaidi ya 200.

Akiongea akiwa katika daraja la Rungwa ambalo ni mpaka kati ya Singida na Mbeya Mkuu wa Mkoa amesema barabara hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi kwa kuwa inaunganisha mikoa mitatu ya Mbeya, Singida na Tabora ambapo itasaidia kuongeza mzunguko wa kibiashara katika  mikoa hiyo.

Amesema kukamilika kwa Barabara hiyo kunatoa fursa ya kuunganisha Tanzania, Zambia na Malawi ambazo zote zinatumia nchi za maziwa makuu kufanya Biashara ikiwa ni pamoja na  nchi nyingine za Afrika mashariki ambapo zitaongeza muingiliano wa shughuli za kibinamu.

Amesema utunzaji wa Mazingira utasaidia kulinda kingo za mito zisiweze kuvunja barabara ambapo amesema kwa kutunza Mazingira kutasaida kupata fedha za kigeni kwa kupunguza hewa ya ukaa Nchini.

Akimnukuu Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu, MKuu wa Mkoa wa Singida amesema  Tanzania imeingia makubaliano ya kutunza na kuhifadhia Mazingira ambapo mikataba mbalimbali imesainiwa hivyo ni jukumu la kila mtanzania kutunza na kuhifadhia mazingira.

Amewakumbusha wananchi kutuza Mazingira  kwa kupanda miti katika maeneo yote ili kuzuia uchepushaji wa maji ya mvua ambayo yamekuwa yakiharibu Barabara.

Aidha ametoa wito kwa wakandarasi hao kuhakikisha kila mmoja anamaliza kazi yake kabla ya kuingia katika kipindi cha mvua nyingi  ili kutozuia shughuli mbalimbali za wafanyabiashara na wasafiri.

Awali akieleza Hali ya mradi huo Mhandisi Matare Masige, Meneja wa TANROAD Mkoa wa Singida amesema Mradi unagharimu kiasi cha sh.Bilion 1.5 na unatekelezwa na wakandarasi watatu na utawasaidia wananchi wa mikoa ya Sikonge, Manyoni na Mbeya pamoja na mikoa ya jirani.

Amesema barabara hiyo imegawanywa katika vipande vitatu kulingana na idadi ya wakandarasi ambao ni M/s Jam Engineers ambayo italipwa kiasi cha sh.milioni 348.3 na M/s Madata In.Ltd ambayo imeingia mkataba wa Milioni 592.7 wakati Kampuni ya M/S JP Treders Ltd imeingia mkataba wa Sh. Milioni 567.93

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba wakati wa ziara ya ukaguzi wa barabara ya Rungwa - Itigi iliyofanyika hivi karibuni

Meneja wa TANROAD Mkoa wa Singida Mhandisi Matare Masige (kushoto) akielezea jambo wakati wa ziara.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.