Wawekezaji mkoani Singida wametakiwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya wakati wa kuanzisha miradi ya Maendeleo ya Kijamii (Community Socially Responsibility – CSR) ili kukubaliana aina za miradi na namna itakavyotekelezwa lengo likiwa ni kuepuka matumizi makubwa ya fedha kwa kazi ambazo zingetumia fedha kidogo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Satano Mahenge akizungumza wakati wa ziara
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Satano Mahenge leo January 26, 2022 alipotembelea machimbo ya madini ya dhahabu yanayochimbwa na kampuni ya Shanta Gold iliyopo kijiji cha Mang’onyi wilayani Ikungi ambapo alieleza kwamba miradi yote inayoanzishwa na wawekezaji ipitie katika Halmashauri za Wilaya ambazo zinafahamu mahitaji ya wahusika na gharama halisi za ujenzi katika maeneo hayo.
Akitolea mfano kwa madarasa yalikamilika hivi karibuni kupitia fedha za uviko 19 RC Mahenge amesema kila darasa liligharimu kiasi cha shilingi milioni 20, ikilinganishwa na madarasa yaliyojengwa na Shanta Gold ambayo yamegharimu Tsh.milioni 28 kwa kila darasa.
“Kama mradi huu mngeshirikisha Halmashauri kwa kiasi kikubwa mngetumia Force Account na mgepata wakandarasi wa bei ndogo na fedha zingebaki zikafanya maendeleo mengine katika jamii. Niwashauri mshirikiane ipasavyo na Halmashauri kupanga aina ya miradi mnayotaka kuipeleka kwa jamii”, alisema Rc Mahenge.
Hata hivyo RC Mahenge akaipongeza Kampuni hiyo ya Shanta Gold kwa kutumia zaidi ya Milioni 190 kwa kupeleka huduma kwa jamii ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na uchimbaji wa visima vya maji huduma ambazo zinafaidisha vijiji vya Mang’onyi, Sambaru, Mlumbi, Tupendane na Mwau.
Aidha, Dkt. Mahenge akaitaka jamii inayozunguka mgodi huo kutumia fursa na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku na mama lishe pamoja na kuomba ajira katika kampuni hiyo kwa kuwa kadri mradi unavyokuwa ndivyo mahitaji yatakavyoongezeka.
Meneja wa Mradi Bw. Kundael Mtiro akitoa taairifa ya mgodi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya kuwasili katika Mgodi huo.
Awali akitoa taairifa ya mgodi Meneja wa Mradi huo Kundael Mtiro amesema mpaka kufikia sasa mradi ulitakiwa kufikia asilimia 46.14 katika utekelezaji wake lakini kwa sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo mpaka sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 43.62 .
Hata hivyo Mtiro akaendelea kufafanua kwamba mpaka June, 2022 mradi utakuwa unakamilisha robo ya nne ya mwaka ambapo wanategemea kwamba utakuwa umekamilika kwa kuwa tayari washasimika mabomba katika maeno yote yanayohusika pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa ofisi na makazi umekamilika kwa asiliami 80.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza wakati wa ziara hiyo
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro amesema mgodi huo utainua uchumi wa Singida na taifa kwa ujumla ambapo utasisimua sekta nyingine za elimu barabara, zahanati na wananchi kupata ajira.
Amesema Wilaya imeendelea kusimamia hali ya usalama katika eneo la mradi na imehakikisha wanachi wote waliokuwa wanastahili kupata fidia zao wamelipwa kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice L. Kijazi (katikati) akizungumza wakati wa ziara hiyo . Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Moja ya darasa la Shule ya Msingi lililotembelewa wakati wa ziara hiyo
Mkuu wa Mkoa (waliosimama mbele wa nne kutoka kushoto) akionyeshwa moja ya eneo linalotumika katika shughuli za machimbo
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.