Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Doroth Mwaluko wakati akitoa miongozo mbalmbali katika kikako kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa ambacho kilichowakutanisha Wakuu wa wilaya na Wakurungezi wa Halmashuri zote za Mkoa wa singida.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Singida wametakiwa kukamilisha jumla ya vyumba vya madarasa 662 na mabweni mawili (2) kabla ya kufikia katikati ya mwenzi Decemba 2021 ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kidato cha kwanza mwaka 2022.
Hayo yamebinishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo 01.11.2021 katika ukumbi wa mikutano ofsini hapo ambapo aliwakutanisha wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida .
Amesema Serikali imetoa fedha za maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 330 ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kidato cha kwanza mwaka 2022 na vyumba 332 vya madarasa vitakavyo gharimu jumla ya shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ujenzi wa vituo shikizi vya shule za msingi .
Hata hivyo Mkuu wa mkoa amebainisha kwamba katika fedha za maendeleo zilizokuja jumla shilingi milioni 160 zitatumika kujenga mabweni mawili (2) katika shule za msingi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Amesema katika kutekeleza mpango wa maendeleo kwa usatwi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19, Mkoa umetengewa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 27.068 kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta ya Afya, elimu na maji.
Hata hivyo Dkt. Mahenge amewataka Wakurugezi wa Halmashauri ya Itigi na Mkalama kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu fedha ambazo zilikuwa bado hazijaingia katika baadhi ya mashule ziweze kuingia na kufanyiwa kazi iliyokusudiwa.
Dkt. Mahenge amewakumbusha viongozi wote wa Hamashauri za wilaya kutosafiri kipindi hiki cha utekelezaji wa miradi hiyo ili kuimarisha usimamizi kama muongozo wa awali ulivyotolewa aliendelea kusema Mkuu wa Mkoa huo.
Akimalizia maagizo yake Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashuri hizo kufanya manunuzi ya pamoja (bulk procurement) ili kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi hiyo na kuwahimiza Mameya wenyeviti wa Halmashuri, watendaji wa Halmashauri na madiwani kusimamia miradi hiyo Kikamilifu.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Doroth Mwaluko akawakumbusha Wakurugenzi hao kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Ofis ya Rais Tamisemi juu ya maandalizi ya utekelezaji wa mpango kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya uviko 19.
Bi. Doroth akatumia muda huo kuagiza kuundwa kwa timu maalum za mkoa na Halmashauri ambazo zitakuwa zikifuatilia miradi hiyo ya maendeleo ya Afya, Elimu na Maji kama maagizo yalivyotolewa na Wizara ya Tamisemi.
Aidha akawakumbusha kuhakikisha miradi yote inayokamilika pamoja na ununuzi wa vifaa unawekwa alama ya mpango wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO -19 ili kuzitambua na kuweza kutofautisha.
Tovuti za Halmashauri pamoja na Mkoa zitumike kikamilifu kutangaza kazi za utoaji wa huduma kwa wanunuzi wa Vifaa na mafundi ili atakayeweza kutoa huduma stahiki apate fursa hiyo, alikaririwa Bi Doroth Mwaluko.
Awali katika wasilisho lake Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na uratibu Bi Beatrice Mwinuka akabainisha kwamba katika jumla ya fedha zote zilizokuja wametanga shilingi bilioni 13.4 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu msingi ambayo ndiyo itakayotumika katika ujenzi wa vyumba 632 na mabweni mawili (2) .
Aidha akaendelea kufafanua kwamba jumla ya shilingi bilioni 9.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na ufuatiliaji wa Afya ya msingi ambapo kutakuwa na ujenzi na ununuzi wa vifaa vya huduma ya dharula (EMD),ujenzi wa majengo ya wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na unuuzi wa X-rays
Beatrice akaendelea kueleza kwamba fedha hizo zimetengwa kwa ajilia ya uboreshaji wa miradi tisa (9) ya maji itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.04 katika wilaya ya Iramba , Mkalama, Singida Ikungi, Manispaa ya Singida pamoja na wilaya ya Manyoni.
MWISHO
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.