• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Mahenge Azindua Rasmi Kampeni ya Usafi Mkoa wa Singida

Posted on: October 30th, 2021

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Binilith Mahenge leo October 30 2021 amezindua kampeni ya usafi Mkoani hapa kwa kufanya usafi Katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Singida ambapo amesema usafi huo utafanyika kila Siku ya  Juma mosi .
Amezindua Kampeni hiyo ikiwa ni siku ya  kumi na mbili tangu alipotoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida  kufanyika usafi kwenye fukwe za maziwa ya Singidani na Munangi wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya mwanzoni mwa mwezi huu.
Akizindua kampeni hiyo Katika ziwa Kindai ambapo aliungana na wananchi kufanya usafi Dkt. Mahenge amesema  ni jukumu la watu wote kuhakikisha kwamba Singida inakuwa Safi  Kama njia ya  kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Awali akisoma Taarifa Mkuu wa Idara ya mazingira  Halmashauri ya Manispaa  Arafa  Mohamedi amesema  lengo la kuzindua  kampeni ya usafi  wa mazingira ni kukumbushana na kuelimisha  kuhusu wajibu  wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha  Arafa  amesema   suala la  uzururishaji  ovyo wa mifugo katikati ya mji ni tatizo lingine linalosababisha uharibifu na uchafuzi  wa  mazingira ongezeko la watu na utiririshaji  wa  maji machafu katika  mitaro na mifereji  wakati wa mvua.
Alisema zipo jitihada  zinazofanywa na Halmashaurj ya Manispaa ya Singida  katika kukabiliana na changamoto za uchafuzi wa mazingira lakini kikubwa ni kuendeleza  juhudi  zilizoanzwa za kampeni ya usafi wa mazingira.
 
Naye Mstahiki Meya wa  Halmashauri  ya Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu  alisema kuwa wao kama Halmashauri  watahuisha timu zote ili kuweka  ulinzi wa Maziwa yasiendelee kuharibiwa na kuvamiwa na wananchi kwani maziwa hayo  ni fahari ya Singida. 
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida  Zefrin  Lubuva alisema kuwa  Halmashauri ya Manispaa  ilipokea maagizo ya Mkuu wa Mkoa  ya kusafisha fukwe  za maziwa yote.
" Sisi Halmashauri ya Manispaa ya Singida pamoja na wananchi  tulipokea  maagizo yako na tunashukuru kwa kutuzindulia kampeni hii ya usafi wa mazingira   na maono yako ya Singida  safi inawezekana yatatimia",alisema  Lubuva"
Aidha Mkuu wa Mkoa  wa Singida Dkt. Binilith Mahenge   wakati akizindua kampeni hiyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halimashauri ya Manispaa ya Singida kusimamia sheria ndogo kwa wale watakao ingiza mifugo katika maziwa hayo.
"Mkurugenzi kuanzia leo ni marufuku watu kuingiza ng'ombe kuona ng'ombe kuzagaa kandokando ya maziwa yetu kwa sababu taratibu unazo  wewe ni kuwatwanga faini tu  hatutaki kuona mifugo kwenye maziwa yetu",alisema Mahenge"
Alisema kuwa maziwa hayo ni chanzo kizuri cha mapato  kwa wale watakao kaidi agizo hilo ni kupigwa faini ya shilingi elfu hamsini  huku elfu kumi ikibaki wa mgambo na elfu 40 kuingia kwenye mapato ya Halmashauri.
Aliongeza kuwa  ni marufuku kwa wananchi kujenga vyoo ndani ya mita 60 kutoka kwenye ziwa ili kutunza mazingira na usafi wa maziwa  pamoja na walaji wa samaki wanaopatikana katika maziwa hayo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.