• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC NCHIMBI ABAINISHA KUSHINDWA KUMPATIA CHANJO MTOTO NI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

Posted on: April 25th, 2017

Wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto kupata huduma za chanjo wanakiuka haki za binadamu hasa haki ya kuishi na pia wanaenda kinyume na juhudi za serikali za kupambana na maradhi, umaskini na ujinga.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesea hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo uliofanyika mapema leo katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida.

Dkt. Nchimbi amesema watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanapaswa kupata chanjo zote ili kuwakinga na magonjwa ya homa ya ini, surua, nimonia, kuhara, kifua kikuu, pepopunda  na magonjwa mengine ambayo yanazuilika kwa chanjo na motto akiugua kupona ni nadra.

“Mtoto akiumwa magonjwa hayo kwa kukosa chanjo kupona ni majaliwa na akipona anaweza kupata ulemavu wa kudumu, hivyo nawasisitiza msipuuze mzingatie kukamilisha chanjo zote” amesisita.

Ameongeza kuwa serikali imekamilisha wajibu wake kwa kuhakikisha chanjo zote zinapatikana na hivyo umebaki wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha mtoto anapata chanjo pamoja na kuwaelimisha na kuwafichua wale wasiowapeleka watoto kupata chanjo.

Akisoma taarifa ya hali ya chanjo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Salum Manyatta amesema Mkoa wa Singida kwa sasa una chanjo zote zinazohitaji na zinatolewa katika vituo 197 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni katika wiki hii ya chanjo.

Dkt. Manyatta amesema kwa mkoa wa Singida wananchi wana uelewa wa chanjo ambapo kila mwaka zaidi ya asilimia 95 hufikiwa na chanjo karibia zote huku changamoto ikiwa ni katika kukamilisha chanjo ambazo huhitaji dozi zaaidi ya moja.

Ameongeza kuwa baadhi ya wazazi hujifungulia nje ya vituo vya kutolea huduma za afya mfano majumbani na hivyo kupelekea watoto kukosa chanjo za awali.

Dkt. Manyatta amesema katika kukabiliana na changamoto za baadhi ya watoto kukosa chanjo, jitihada zilizowekwa ni pamoja na kupitia kadi ya mtoto kuona endapo amekamilisha chanjo kabla hajapewa huduma nyingine za afya.

Jitihada nyingine ni viongozi wa serikali ngazi za vijiji watapewa orodha ya watoto ambao hawajakamilisha chanjo kutoka katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wawafuatilie wazazi au walezi wakamilishe chanjo hizo pia kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa chanjo na kutoa huduma ya mkoba na kliniki tembezi ili kuwafikia watoto wanaoishi maeneo ya vijijini sana.

Kauli mbiu ya wiki ya chanjo mwaka huu ni “Chanjo Humkinga Kila Mtu, Pata Chanjo”.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.