• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Serukamba aagiza Vyama vya Ushirika viimarishwe ili kujenga uchumi wa Mkoa

Posted on: October 13th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameagiza kuanzishwa na kuimarishwa vyama vya Ushirika  Mkoani hapo  ili viweze kutoa huduma kwa wananchi na kutatua changamoto za soko pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma mbalimbali katika maeneo husika.

Rai hiyo ameitoa leo 13 Octoba, 2022 akiongea na wanaushirika katika jukwaa la Maendeleo ya Ushirika lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhasibu Mkoani hapo.

RC Serukamba ameeleza kwamba  Sekta za kipaumbele na kiuchumi katika Mkoa wa Singida ni kilimo, madini na ufugaji na vyanzo vikuu vya mapato katika Mkoa wetu. Hivyo ni muhimu kuvitambua vipaumbele katika kuanzisha na kuimarisha Vyama vya Ushirika katika sekta ya kilimo, ufugaji na madini ili viweze kutoa huduma kwa wananchi kama inavyotarajiwa.

"Ninawaelekeza Wakurugenzi wote kwa kushirikiana na Mrajishi wa Vyama vya Ushirika na Maafisa Ushirika katika Halmashauri kuweka mpango katika kila Halmshauri kuanzisha Vyama vya Ushirika vya aina mbalimbali kwa kuanzia na mazao ya kimkakati Korosho, Mkonge, Tumbaku na Alizeti, sambamba na kuimarisha vyama vya Ushirika vilivyopo katika maeneo yenu". Alisema Serukamba.

Serukamba alibainisha kwamba Serikali inahimiza uanzishwaji wa Vyama imara katika sekta mbalimbali za kiuchumi vinavyotoa matarajio ya wanachama ikiwa kama nyenzo muhimu ya Maendeleo.

Aidha, Vyama vya Ushirika vinapaswa vitumike kuchochea kasi ya Maendeleo ya Taifa na hivyo kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi katika Mkoa wa Singida.

Hata hivyo amewataka Viongozi na Watendaji wote wa Vyama vya Ushirika kusimamia na kuendesha vyama hivyo kwa kuzingatia sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013, Sheria ya huduma ndogo za Kifedha ya mwaka 2018 na kanuni zake wakati wote wa uendeshaji wa vyama vya Ushirika na kujiepusha na ubadhirifu, wizi, matumizi mabaya ya madaraka, kutokuwajibika na uzembe kwa kuwa vitendo hivyo vinasababisha Vyama vya Ushirika kuendelea kuzorota na kushindwa kutoa huduma kama ilivyotarajiwa.

Serikali ya awamu ya sita haitawavumilia kamwe viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika watakaofanya ubadhirifu, wizi na kusababisha hasara katika Vyama vya Ushirika  na kwamba yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuondolewa madarakani, kufikishwa Mahakamani na kufidia hasara zote zitakazojitokeza.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.