• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Serukamba amewataka wakulima waliopewa mashamba kwenye Skimu ya umwagiliaji Itagata kuyaendeleza haraka mashamba hayo.

Posted on: August 11th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka wakulima waliopewa mashamba kwenye Skimu ya umwagiliaji Itagata katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi mkoani Singida kuyaendeleza  haraka mashamba hayo kwa kuyalima mazao yenye tija kwa mtu binafsi na Serikali vinginevyo Serikali itawanyang'anya na kuwapa watu wengine.

RC Serukamba amesema hayo baada ya kufanya ziara ya kikazi kukagua shughuli za kilimo zinazofanywa na wakulima kwenye skimu hiyo ambayo imeigharimu Serikali bilioni 2.1 hadi kukamilika kwake.

Akiwa katika mashamba ya wakulima kwenye skimu  ya Umwagiliaji Itagata Itigi RC Serukamba amesikitishwa na kilimo kinavyoendelea ambapo kati ya ekari 209 walizogawiwa wakulima ambao ni wananchama wa umoja wa umwagiliaji Itigi ekari 40 tu ndizo walizolima muda wa kiangazi jambo ambalo amesema halitakubalika.

"Serikali imewekeza fedha nyingi sana kwenye mradi huu na mimi nimefika kwenye mashamba haya nimeyaona, watu wengi hawajalima kuna jumla ya ekari 209 lakini ekari zilizolimwa kiangazi hiki ni 40 tu mashamba na maji yapo, sasa hii haikubaliki lazima watu walime ili kuisaidia Serikali kupata mapato, Tume ya umwagiliaji nao wapate tozo zao" alisema Serukamba

Aidha Mhe. Serukamba ameongeza kwa kuwataka wananchama wote wa ushirikia kuandaa mkutano ambao  utakuja kubainisha na kuwatambua wakulima waliopewa mashamba, na ambapo wanalima kutumia skimu hiyo.

"Mwezi wa tisa mwenyekiti andaa mkutano na wanachama wako ili tuje tujue nani analima na nani halimi ili wale ambao hawalimi tuwaondolee mashamba tuwape wengine ambao watalima na kuipa Serikali mapato pamoja na Tume ya umwagiliaji" Aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa Singida

Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa faida atakayoipata mkulima kupitia kilimo kwenye skimu hiyo itamrahishia maisha kiuchumi ataweza kuhudumia familia, kulipa bima ya afya  pamoja na kuchangia maendeleo ya taifa lake.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa mkulima anayejulikana kama Chacha Marwa alisema kuwa changamoto mojawapo inayopelekea  wakulima wengi kutolima ni kushindwa kutambua aina ya udongo  pamoja na baadhi ya Wanachama  wa umoja huo wa umwagiliaji waliopewa mashamba kuyakodisha kwa watu wengine.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa sisi huu udongo unatuchanganya sana tunashindwa kuelewa tulime mbegu gani tunaomba mtusaidie kutupimia udongo wetu" Alisema Chacha.

Aliongeza kuwa baadhi ya wasimamizi wa skimu hiyo sio waaminifu kwa wanachama wao jambo linalopelekea washindwe kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji akisema kuwa baadhi wamekuwa wakikodisha mashamba na kuwanyima fursa wengine.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mwenyekiti wa Umoja wa umwagiliaji Itagata Stephen Mbonge alisema kuwa mashamba yenye ukubwa wa Ekari 209 yaligawiwa kwa wanachama 321 ekari 106 ziligawiwa kipindi cha masika mbunga ekari 73 na kutoa tani 105.7 na mazao mengine ekari 33 ambazo zimetoa tani 28.19 lakini kipindi hiki cha kiangazi ekari 40 tu ndizo zimelimwa zikiwa na mazao mchanganyiko na hazijavunwa.

Baada kusomewa taarifa ya mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Mkuu wa Mkoa Serukamba akafika  kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Itagata msisitizo wake ukiwa katika kuendeleza mashamba yaliyopo kwenye skimu hiyo, kushiriki kwenye zoezi la Sensa Agosti 23 mwaka huu na kuwataka wananchi wa kijiji chicho kukata Bima ya afya ambayo imekuwa ndio wimbo wake tangu aanze majukumu yake Mkoani Singida.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.