• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SERUKAMBA ASISITIZA MARUFUKU MALORI KUPAKI PEMBEZONI MWA BARABARA MANYONI

Posted on: July 26th, 2023

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesisitiza kuwa  uamuzi alioutoa wa kutaka malori inapofika saa 2:00 usiku yapelekwe kuegesha kwa ajili ya kulala katika stendi ya Manyoni utabaki kama ulivyo kwa kuwa umesaidia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kupata mapato kutokana na ushuru wa magari hayo.

Ametoa msisitizo huo wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika hivi karibuni katika kitongoji cha Majengo Kata ya Manyoni ambao wananchi walimweleza kuwa uamuzi wa kupiga marufuku malori yasiwe yanaegeshwa pembezoni mwa barabara kumeathiri biashara zao.

Mhe. Serukamba alisema kuanzia asubuhi hadi saa 2:00 usiku ni ruhusa malori kupaki pembenezoni mwa barabara lakini baada ya muda huo yapelekwe stendi ambako yatalazimika kulipa ushuru wa stendi wa Sh. 3,000 kwa kila gari fedha ambazo zinaingia halmashauri na kusaidia kwa ajili ya maendeleo.

Alisema kimsingi wanaolalamikia suala hilo ni wale ambao walikuwa wakinufaika binafsi na malori yanapopaki pembezoni mwa barabara ambapo fedha za ushuru zilizokuwa zinatolewa na wenye magari zilikuwa zikiwanufaisha wao binafsi na hivyo halmashauri kukosa mapato.

Serukamba alisema kabla ya kuweka utaratibu huo miezi miwili iliyopita, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ilikuwa ikipata ushuru Shilingi Milioni mbili tu kwa mwezi kutokana na ushuru wa malori kupaki pembezoni mwa barabara  lakini hivi sasa kwa mwezi zinakusanywa zaidi ya Shilingi milioni 4 kwa mwezi ambazo zinaingia moja kwa moja halmashauri.

Aidha, Mkuu wa Mkoa aliendelea kuwakumbusha wafanyabiashara wote mkoani Singida kuhakikisha wanalipa kodi ili Serikali iweze kupata mapato ambayo yatatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota akizungumza wakati wa mkutano huo

Mkurugenzi wa Manyoni JIMSON PETER MHAGAMA akizungumza wakati wa mkutano huo

 Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Manyoni akizungumza wakati wa mkutano huo 

 


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.