• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SERUKAMBA ATOA AGIZO MIRADI INAYOTEKELEZWA WILAYANI MKALAMA IKAMILIKE IFIKAPO JUNI 20, 2023

Posted on: May 26th, 2023

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameanza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Mkalama na kutoa agizo kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha ifikapo Juni 20, mwaka huu iwe imekamilika.

Pia ametoa agizo baadhi ya miradi kama ya ujenzi wa shule mpya za msingi  ujenzi uwe unafanyika kwa saa 24 na kuongeza idadi ya mafundi ili kuongeza kasi ya ujenzi na kumwagiza Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) Wilaya ya Mkalama kupeleka umeme kwenye miradi hiyo ili kuwezesha mafundi kufanya kazi muda wote.

Ametoa agizo hilo leo (Mei 26, 2023) katika siku ya kwanza ya ziara yake Wilayani Mkalama ambapo alitembelea na kukagua miradi sita ambayo ni ujenzi wa shule mpya za msingi, ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa, vyoo, zahanati na Hospitali ya Wilaya ya Mkalama.

Serukamba alianza kwa kutembelea kikundi cha watu wenye ulemavu Iguguno kinachojishughulisha na biashara ndogondogo, ukamlilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Lukomo na ujenzi wa shule mpya ya msingi Ishenga.

Akiwa katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Ishenga alimwagiza Mhandisi wa Wilaya kuhakikisha kila siku awe anafika kwenye mradi huo kukagua kuona ujenzi unavyoendelea na atembelee kila jengo kujua changamoto iliyopo kwa mafundi na kuitatua.

“Mhandisi wa Wilaya kwanza wewe ubaki hapa hapa kwenye mradi hakuna haja ya kuendelea na mimi kwenye ziara baki usimamie tunataka mradi huu ifikapo Juni 7, mwaka huu ujenzi wa shule hii uwe umekamilika,” alisema Serukamba.

Katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuari ya Wilaya ya Mkalama ambayo Serikali imeshatoa Sh. Milioni 300, aliagiza ifikapo Juni 20, mwaka huu ujenzi uwe umekamilika na kukabidhiwa kwa Serikali.

Mkuu wa Mkoa akiwa katika mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo 17 shule ya msingi Mazilinga alimwagiza Afisa Elimu Shule za Msingi kuhakikisha anasimamia kwa karibu ujenzi huo na uwe umakalimika ifikapo Juni 19, mwaka huu.

Aidha, Serukamba alitoa agizo la jumla kwa Mhandisi wa  Ujenzi wa Mkoa katika shule tisa mpya za msingi zinazojengwa kwenye Halmashauri kutokana na fedha za mradi wa BOOST kuanzia Jumatatu wiki ijayo aanze kuitembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi na siku ya Ijumaa ampelekee ripoti.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.