• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SINGIDA APONGEZA HALMASHAURI ZA MKOA WA SINGIDA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018.

Posted on: June 13th, 2019

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amezipongeza Halmashauri zote za mkoa wa Singida kwa kupata hati safi, kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Dkt. Nchimbi, ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika kikao Maalum cha Baraza la Madiwani cha hoja za ukaguzi kilichofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida.


Amesema, Watumishi na Watendaji  ni waajiriwa wa Serikali  iliyoko madarakani, ni lazima wawe waaminifu na waadilifu kwani ndiyo inayowalipa mshahara.


‘’Ukiona mahali kuna hoja za ukaguzi, ujue kiwanda cha kuzalisha  hoja ni watumishi na watendaji,  sisi watumishi na watendaji tukikaa vizuri hakutakuwa  na hoja, ninyi ambao hamkuwepo wakati hoja za ukaguzi zilipokuwa zinazalishwa na watendaji waliopita onyesheni mfano basi msiwe na dhana ya kukariri, kunakilishwa halafu ninyi wenyewe hamuonyeshi mabadiliko, hivyo inawapasa kuonyesha kwamba sisi hatuna hoja ndipo hapo tutakapokutana na kujipongeza kwamba tumepata hati safi’’ Dkt. Nchimbi


Amesema, ni lazima watumishi na watendaji wazingatie hasa kwa utumishi wa awamu ya tano, awamu ambayo si ya maslahi binafsi bali ni ya  kutekeleza agenda za kitaifa.


‘’Sisi sote ni wasaidizi wa Mheshimiwa. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais ambaye hafanyi kazi kwa maslahi yake, hivyo inawapasa kuwa makini sana katika utendaji  wenu”. Amesisitiza Dkt. Nchimbi


Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida amezipongeza kwa dhati Halmashauri zote za Mkoa wa Singida kwa kupata hati na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuwatumikia Wananchi na Taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi, amesema kuwa kuna hoja zingine  hazikuwa za lazima bali ni uzembe wa watendaji  ambao hawakuwa makini  katika kutekeleza majukumu yao.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Bw. Linno Mwageni, aliwasilisha hoja za ukaguzi 64  na kutoa taarifa ya Halmashauri hiyo kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.


IMETOLEWA NA, 

KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO

OFISI YA MKUU WA MKOA

SINGIDA

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.