• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SINGIDA, SITAKI KUONA WANAFUNZI WANAKAA CHINI KWA KUKOSA MADAWATI SHULENI, WAKURUGENZI SIMAMIENI HILO.

Posted on: May 24th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri Saba za mkoa huo kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa haraka kwenye shule za Msingi na Sekondari ili kujua hali ya uhaba wa madawati ilivyo na kuchukua hatua ya kuondoa tatizo la Wanafunzi kujisomea wakiwa wamekaa sakafuni haraka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Halima Dendego ametoa kauli hiyo leo (24 Mei, 2024) wakati akizungumza na Viongozi wa Manispaa ya Singida na Walimu wa shule ya Msingi Bomani iliyopo Manispaa ya Singida baada ya kufanya ziara ya kustukiza kwenye shule hiyo kufutia kusambaa kwa picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha wanafunzi wa shule hiyo wakifanya mtihani yao wakiwa wamekaa chini.

RC Dendego, amesema picha hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimesababisha taharuki kubwa kwa jamii tofauti na hali ilivyo kwenye shule hiyo ambayo inaupungufu wa madawati Nane (8).

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida pia ametoa siku Saba (7) kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kuhakikisha anapeleka madawati Nane yanayohitajika kwenye shule hiyo ili wanafunzi wa shule hiyo ya Bomani waweze kujifunza na kujisomea katika hali bora na nzuri zaidi.

Naye, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bomani Joachim Msechu, amesema sio kweli kuwa shule hiyo inaupungufu mkubwa wa madawati na upungufu uliopo ni madawati Nane tu na walikuwa kwenye mchakato wa kukarabati madawati mengine yaliyoharibika ili wanafunzi waweze kuyatumia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe, amemhakikishia Mkuu wa mkoa huo kuwa maelekezo aliyoyatoa watayafanyia kazi kuanzia sasa ili kuondoa mapungufu madogo madogo yanayotokea kwenye sekta ya elimu ili kuimarisha shughuli za ufundishaji wa wanafunzi mashuleni.

Kwa sasa shule ya msingi Bomani iliyopo katika Manispaa ya Singida ina wanafunzi 894 na walimu 16.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.