• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Serikali Imeupatia Mkoa wa Singida Sh.Bilioni 5.8 Kujenga Vyumba vya Madarasa 290

Posted on: November 1st, 2022

SERIKALI imeupatia Mkoa wa Singida Sh.Bilioni 5.8 ambazo zitatumika kujenga vyumba vya madarasa 290 kwa ajili ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza kuanzia Januari 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, alisema hayo hivi karibuni wakati wa kuwekwa Wakfu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati, Askofu Dk. Syprian Hilinti.

Kufuatia hali hiyo, aliwagiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kuwapeleka watoto wao shule watakaoanza darasa la kwanza na wale wa kidato cha kwanza kwani Serikali imeweka mazingira mazuri ya kumuwezesha kila mtoto anapata elimu.

Serukamba ambaye alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla hiyo, alisena Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Kanisa la KKKT katika huduma ya Kiroho na kuhubiri Injili ya amani, umoja, upendo na katika kulea na kukuza vipawa mbalimbali.

"Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati pia linatoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu na afya kwa kushirikiana na Serikali, mfano mmojawapo ni hospitali ya Iambi iliyopo Wilaya ya Mkalama ambayo inamilikiwa na Kanisa hilo ambapo Serikali inalipa mishahara ya watumishi  31 ili kuyawezesha malengo ya Kanisa katika utoaji huduma kwa wananchi," alisema.

Kuhusu kufunguliwa njia ya reli ya kutoka Manyoni kuja Singida, alisena Serikali ya mkoa ilishawasilisha ombi hilo kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ajili ya kufufua njia hiyo na shirika limeahidi kushughulikia.

Alisema katika suala la ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa upo katika mpango wa Serikali ambapo mkoa ulipokea maelekezo ya kubainisha eneo ambapo uwanja utajengwa.

Alisema changamoto iliyopo ni kwamba eneo la uwanja wa ndege wa sasa limevamiwa na kujengwa nyumba za makazi jambo ambalo linaunyima sifa uwanja huo kutengenezwa kwa hadhi na kiwango cha kisasa.

"Eneo la pili lililobainishwa na kutengwa Kijiji cha Manga linahitaji malipo makubwa ya fidia ili wananchi waliomo ndani ya eneo hilo wapishe kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege," alisema.

Hata hivyo, alisema suala hilo bado Serikali inaendelea nalo na ana imani jawabu litapatikana kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa hasa kwa kuzingatia jiografia ya Mkoa wa Singida ambao ni jirani ya makao makuu ya nchi.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya Singida – Hydom – Mbulu alisema  ipo kwenye mpango na utekelezaji wake umeanza ambapo kipande cha Singida – Ilongero – Hydom chenye urefu wa KM 93.3 kazi ya upembuzi yakinifu na maandalizi ya kutangaza zabuni zinaendelea.

Aidha, aliwagiza wakuu wa Wilaya za Singida na Iramba kushughulikia migogoro ya ardhi maeneo ya Kititimo, Ruruma na Ushora na kumpa taarifa ifikapo Novemba 30, mwaka huu ambao Kanisa la KKKT lililalamika kuwa maeneo hayo ambayo ni mali ya Kanisa yamevamiwa.

MWISHO

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.