• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Serikali kutenga Sh.Bilioni 4.6 kwa ajili ya kununulia zana za kilimo Mkoa wa Singida kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Posted on: October 6th, 2022

SERIKALI katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2023/2024 inatarajia kutenga Sh.Bilioni 4.6 kwa ajili ya kununua zana za kilimo Mkoa wa Singida.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameyasema hayo kwenye kikao cha kupanga mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti kilicho washirikisha Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa kilimo ambacho kiliketi leo Oktoba 5, 2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Alisema Serikali baada ya kununua zana hizo halmashauri zitatakiwa zitenge maeneo maalumu ambapo zana hizo zitawekwa na kutakuwepo mtu maalum wa kuzisimamia na wakulima watakuwa wakienda kukodisha.

Alisema fedha zitakazopatikana baada ya wakulima kukodi zana hizo zitarudishwa Serikalini na kwenda kununua zana hizo katika mikoa mingine.

Awali akitoa mchanganua wa bajeti ya ununuzi wa zana hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mkakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo Justice Kijazi alisema Halmashauri za Wilaya za Ikungi, Mkalama, Iramba na Itigi kila moja zitahitaji zana zenye thamani ya Sh.706 Milioni.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni itahitaji Sh.791Milioni huku Singida DC ikiwa ni Sh.309 Milioni.

Akizungumzia kuhusu mpango mkakati wa zana hizo Kijazi alisema ni kuimarisha upatikanaji wa zana bora za kilimo, mkoa unaboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wa zana za kilimo, kuanzisha vituo vya umahiri wa zana (Agricultural mechanization hub) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo.

Alitaja mkakati mwingine kuwa ni kuwaelimisha wakulima kuhusu mikopo ya kibenki yenye lengo la upatikanaji wa zana bora za kilimo kwa masharti nafuu na Mfuko wa Pembejeo (AGITF) uwezeshe wakulima upatikanaji wa mikopo nafuu ya zana za kilimo mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza wakati wa kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba alisema mkoa umejipanga kusimamia kilimo ili kiwe sababu ya kuondoa umasikini kwa wananchi.

“Mheshimiwa Waziri napenda kukuhakikishia kuwa hapa Singida kazi kubwa ni kilimo tutakifanya usiku na mchana ili tuweze kuwasaidia wananchi wetu na maelekezo yako yote tutayafanyia kazi” alisema Serukamba.

Serukamba alisema awali watu walidhani kuwa kilimo ni jambo la kawaida na la mtu binafsi lakini sasa ni biashara na mkombozi kwa wananchi na kuwa wanazipongeza jitihada zote zinazofanywa na Serikali za kuinua kilimo na wao kama mkoa wanaziunga mkono na kutekeleza maagizo yote waliyopewa.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.